Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Habari Mpya

Maelfu na maelfu ya wakimbizi kupata mikopo

Maelfu na maelfu ya watu walopoteza makazi yao kote duniani watapata mikopo midogo ili kuweza kuanzisha biashara zao wenyewe na kuweza kujitegemea, kufuatia makubaliano kati ya Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji UNHCR na shirika la kutoa mikopo midogo iliyoanzishwa na mshindi wa tunzo ya Nobel Muhammad Yunus kutoka Bengladesh Grameen Trust.

UM unapeleka Msaada wa dharura Haiti

Umoja wa Mataifa umeshafanya uchunguzi wa awali kwa ndege huko Haiti na kugundua kwamba kuharibika kwa majengo na miundo mbinu kumetokea katika maeneo mengi kabisa ya mji mkuu na maeneo ya jirani.

UM:zaidi ya watu milioni 3 wathirika na tetemeko Haiti

Akionekana na huzuni alipokua anazungumza na waandishi habari katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema zaidi ya watumishi 100 wa umoja wa mataifa hawajulikani walipo huko Haiti, na umoja huo unatathmini maafa na hasara zilizopatikana kutokana na tetemeko kubwa la ardhi jana jioni nchini humo.

Mataifa ya dunia kusaidia Haiti

Marekani na mataifa mengi ya kigeni yameshaanza kupeleka msaada wa dharura huko Haiti, Rais Barack Obama ameahidi mpango kabambe wa dharura ukatayo ratibiwa vyema kusaidia Haiti.

IOM inawasaidia wakimbizi wanaorudi Angola

Shirika la kimataifa la wahamiaji IOM, huko Angola litatoa msaada wa dharura kuimarisha usalama wa chakula na viwango vya lishe kwa jamii ambazo zinakabiliwa na hatari kutokana na idadi kubwa ya watu wanaorudi nyumbani na maafa ya kimaumbile.