Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Makala

11-12-2023_FAO_Lopit_South Sudan.jpg

FAO yawashika mkono wasichana Afrika kuingia katika sayansi ya kilimo

Katika kuelekea siku ya kimataifa ya wanawake na wasichana katika sayansi itakayoadhimishwa Jumapili Februari 11 shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa FAO limesema katika Dunia ya sasa inayobadilika kwa kasi, sayansi na ubunifu vina jukumu muhimu katika kushughulikia changamoto zinazoiandama Dunia.

Sauti
4'15"
UNDP/Tanzania

Kampeni ya UNDP Tanzania ya kukabili misimamo mikali yainua vijana kiuchumi Kilwa Masoko mkoani Lindi

Nchini Tanzania, shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo, UNDP linatekeleza mradi wa kukabili misimamo mikali kupitia kampeni ya amani kama njia mojawapo ya kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu, SDGs. Tayari kuna wanaufaika na mmoja wao ni Nuru Mbaruku Ramadhani, mwenyekiti wa kikundi cha Masoko 2 Peace Club kilichoko Kilwa Masoko mkoa wa Lindi, kusini mashariki mwa Tanzania. Kikundi hiki kilichoanzishwa mwezi Juni mwaka 2023, kina mabalozi 9 wa amani wakiwemo wanawake 6 na wanaume 3.

Sauti
5'1"
UN Habitat Mozambique

Mwanafunzi Msumbiji: Iwe mvua iwe upepo mkali madarasa yetu ni salama

Kila mwaka, Msumbiji hukabiliwa na matukio ya hali mbaya za hewa kupindukia kama vile vimbunga na mafuriko, matukio ambayo husababisha uharibifu wa shule na hatimaye watoto kushindwa kujifunza. Hata hivyo, ujenzi wa madarasa yanayohimili matukio kama vile pepo kali na mafuriko umeleta nuru na matumiani kwa watoto, wazazi na walimu. Madarasa haya yanawezesha watoto kubakia salama hata wakati wa mvua na upepo mkali. Hali hii ni uwekezaji wa kudumu kwani ni  hakikisho kwa watoto kuendelea kupata elimu na mustakabali wao kuwa bora.

Sauti
4'11"
© FAO/IFAD/WFP/Eduardo Sotera

Angola: Mradi wa IFAD umeniheshimisha Kijiji kwetu- Albertina

Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Maendeleo ya Kilimo, IFAD ni taasisi ya fedha ya kimataifa na pia shirika la Umoja wa Maitafa lililojikita katika kutokomeza umaskini na njaa kwenye maeneo ya vijijini yaliyoko katika nchi zinazoendelea. Miongoni mwa maeneo ambako Mfuko huo unafanya kazi ni nchini Angola barani Afrika ambako huko takwimu zinaonesha ongezeko la vijana wanaohamia mijini kutoka vijijini kwa sababu ya umaskini wa vijijini.

Sauti
4'36"
World Bank

Nuzulack Dausen: Nishati safi inanusuru mazingira na kuinua kipato katika jamii

Leo ni siku ya kimataifa ya nishati safi ambayo lengo lake ni kuzihimiza jamii kote duniani kutekeleza lengo la 7 la maendeleo la Umoja wa Mataifa la kuhakikisha kila mtu anahamia kwenye matumizi ya nishati hiyo ifikapo mwaka 2030. Nchini Tanzania wako msitari wa mbele katika harakati za utekelezaji wa lengo hilo na miongoni mwao ni Nuzulack Dausen mwanzilishi wa Jukwaa la kidijitali la Jiko point linaloendesha kipindi cha mwanaume jikoni kupitia mtandao wa Youtube.

Sauti
5'1"
UN News

Wakazi wa Ituri, DRC, wazungumzia usaidizi wa MONUSCO kwenye eneo lao

Katika jimbo la Ituri, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, watu waliokimbia makazi yao wanaishi katika takribani kambi 38, ambapo miongoni mwao ni Drodro, Roe, Lodha, Jaiba na Gina. Zaidi ya wakimbizi Laki Nne (400,000) wanafaidika na ulinzi wa moja kwa moja wa ujumbe wa walinda amani wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo, MONUSCO.  Walinda amani hao wakiwemo wale wa kutoka Nepal hulinda kambi za watu waliohamishwa kwa kufanya doria za usiku na mchana.

Sauti
4'24"
IMF/Esther Ruth Mbabazi

EmpowerU Cash+; yabadilisha maisha katika Wilaya ya Lamwo nchini Uganda

Kutokana na ushirikiano kati ya serikali ya Uganda na ya Uholanzi, Mradi wa Maendeleo wa Kukabiliana na Athari za Ufurushwaji (DRDIP), Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) kwa kutumia mfumo wa fedha taslimu wa EmpowerU Cash+.limewasaidia walengwa waliochaguliwa katika Wilaya ya Lamwo ambapo mpango uliwalenga wakimbizi na jamii zilizowapokea.  

Sauti
4'45"
© UNICEF Burundi

Mbinu 3 za kuhakikisha watoto wanapata chanjo

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya watoto ulimwenguni UNICEF linatumia njia mbalimbali kuhakikisha watoto na familia zao wanapata chanjo stahili hili kuwaepusha kuugua magonjwa ambayo mengine yanaweza kuzuilika kwa kupata chango. Katika Makala hii Leah Mushi anatujuza mbinu tatu zinazotumiwa na UNICEF kuhakikisha jamii inapata chanjo. 

Sauti
3'8"