Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Muunganisho wa kijamii huondoa upweke na kuboresha afya kwa jamii – WHO

Muunganisho wa kijamii huondoa upweke na kuboresha afya kwa jamii – WHO

Pakua

Mwezi Novemba mwaka jana shirika la Umoja wa Mataifa la Afya duniani, WHO lilizindua Kamisheni  ya kuchochea Muunganisho wa Kijamii au Social Connection kwa lengo la kuondokana na tatizo la upweke ambalo limetambuliwa kuwa moja ya tishio kubwa la afya duniani. WHO inasema kutengwa na jamii na kuishi maisha ya upweke ni jambo hatari, chungu, na zaidi hatari kwa afya ya binadamu. Upweke  unaweza kuathiri mtu yeyote, wa hali yeyote mahali popote. Kamisheni hiyo sasa kupitia video za Muunganisho wa Kijamii hufikia watu kote ulimwenguni wanaoishi pekee yao lengo kuu likiwa ni kuwapatanisha na kuwashirikisha na jamii pamoja na marafiki ili waondokane na msongo wa mawazo na kuboresha afya yao. 

Tayari msusururu wa video hizo umeanza kuchapishwa mitandaoni ambapo Selina Jerobon wa Idhaa hii amefuatilia simulizi ya Maria Ondosia Mawero, mama mzee anayeishi katika eneo la mabanda la Kibera jijini Nairobi, nchini Kenya akitueleza ni kwa nini uhusiano wa kijamii ni muhimu kwa afya yetu, ustawi na ubinadamu wetu.

Audio Credit
Assumpta Massoi/Selina Jerobon
Sauti
4'6"
Photo Credit
WHO