Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

EmpowerU Cash+; yabadilisha maisha katika Wilaya ya Lamwo nchini Uganda

EmpowerU Cash+; yabadilisha maisha katika Wilaya ya Lamwo nchini Uganda

Pakua

Kutokana na ushirikiano kati ya serikali ya Uganda na ya Uholanzi, Mradi wa Maendeleo wa Kukabiliana na Athari za Ufurushwaji (DRDIP), Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) kwa kutumia mfumo wa fedha taslimu wa EmpowerU Cash+.limewasaidia walengwa waliochaguliwa katika Wilaya ya Lamwo ambapo mpango uliwalenga wakimbizi na jamii zilizowapokea.  

Mpango huo wa EmpowerU Cash+ ulikuwa unalenga idadi ya juu ya watoto kufikia wanne kwa kila kaya na kila mtoto kila mwezi alipewa Shilingi 45,000 za Uganda sawa na takribani  dola 11 za kimarekani hiyo ikimaainisha kila kaya ilipata jumla ya Shilingi za Uganda 180,000 sawa na takribani dola 47 za kimarekani kwa mwezi. Huduma hiyo ilikuwa kwa muda wa miezi sita katika wilaya za Lamwo, Adjumani, Yumbe, na Obongi lakini hapa ninaangazia wilaya moja tu, Lamwo. 

Audio Credit
Anold Kayanda
Audio Duration
4'45"
Photo Credit
IMF/Esther Ruth Mbabazi