Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

FAO yawashika mkono wasichana Afrika kuingia katika sayansi ya kilimo

FAO yawashika mkono wasichana Afrika kuingia katika sayansi ya kilimo

Pakua

Katika kuelekea siku ya kimataifa ya wanawake na wasichana katika sayansi itakayoadhimishwa Jumapili Februari 11 shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa FAO limesema katika Dunia ya sasa inayobadilika kwa kasi, sayansi na ubunifu vina jukumu muhimu katika kushughulikia changamoto zinazoiandama Dunia. Hata hivyo licha ya hatua kubwa zilizopigwa katika kuendeleza sayansi wanawake na wasichana wanaendelewa kukabiliwa na vikwazo vingi kuingia katika tasnia hiyo ndio maana shirika hilo limeamua kuchukua hatua kuendesha mafunzo ya kuwajengea uwezo hususan wasichana katika sayansi ya takwimu katika kilimo. Leo tunakupeleka Côte D’Ivoire  kushuhudia mchango wa FAO katika hilo. Flora Nducha anafafanua zaidi katika makala hii

Audio Credit
UN News/Flora Nducha
Audio Duration
4'15"
Photo Credit
11-12-2023_FAO_Lopit_South Sudan.jpg