Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Makala

Paschal Masalu wa ElimikaWikiendi ahojiwa na Habari za UN

Vijana wana mchango mkubwa katika kusongesha ajenda ya mwaka 2030 ya maendeleo endelevu au SDGs . Hayo yamesisitizwa katika jukwaa la vijana la Umoja wa Mataifa 2018 lililokunja jamvi hii leo kwenye makao makuu ya Umoja huo New York Marekani. Vijana 700 kutoka nchi mbalimbali wamejadili jinsi gani washirikishwe na mchango wao katika kufanikisha azma hiyo ya Dunia. Miongoni mwa waliohudhuria ni kijana Paschal Masalu kutoka nchini Tanzania ambaye ni afisa mtendaji wa jukwaa la Elimikawikiendi nchini humo.

Sauti
3'43"

Ukatili dhidi ya wakawake marufuku Burundi: Seruka

Ukatili wa kijinsia ni changamoto kubwa nchini Burundi huku Zaidi ya asilimia 90 ya wanaotendewa ukatili huo wakiwa ni wanawake na watoto. Sasa shirika lisilo la kiserikali la SERUKA limeamua kushikia bango dhuluma hiyo kwa kuendesha kampeni katika maeneo mbalimbali nchini humo kupinga na kuelimisha jamii kuachana na ukatili dhidi ya wanawake. Mwandishi wetu wa maziwa makuu Ramadhan Kibuga alitembelea moja ya kampeni za shirika hilo kwenye uwanja wa Parke mjini Bujumbura uangana naye kwenye Makala hii.

Ngoma ya vinyago yainyanyua Cote d'Ivoire

Utamaduni ni kielelezo cha utashi wa kila jamii ambapo kupitia utamaduni huo jamii hujielezea ilivyo na kujitambulisha pia kwa jamii zingine. Nchini Cote d' Ivoire katika jamii ya Guro, ngoma yao inayotumia vinyago imekuwa na manufaa kwa jamii na nchi nzima hadi kutambuliwa na Umoja wa Mataifa. Je ni ngoma ya aina gani? Ungana basi na Assumpta Massoi kwenye makala hii.

Kilimo cha kisasa dawa mujarabu ya mabadiliko ya tabia nchi

Ajenda ya maendeleo endelevu ya  mwaka 2030 ya Umoja wa Mataifa  inahimiza nchi zote wanachama kuwekeza katika kilimo cha kisasa ili kukabiliana na changamoto za mbadiliko ya tabia nchi na pia uhabibifu wa mazingira.

Nchini Senegal Afrika magharibu serikali kwa kushirikana na mashirika ya kibinadamu wameitikia wito huo ili kusaidia wananchi katika kutoa elimu ya kilimo cha kisasa katika kupambana na matatizo ya ukame unaokumba nchi nyingi za Afrika zilizoko kusini mwa jangwa la sahara.

Kutoka Nigeria hadi Hungary, kulikoni?

Ama kweli wahenga walinena kuwa mchumia juani, hulia kivulini na methali hiyo imedhihirika kwa raia mmoja wa Nigeria ambaye baada ya kupitia machungu mengi kwenye mikono ya wasafirishaji haramu, sasa ametulia tuli. Ndoto yake ya kufika Ulaya ilitimia na sasa ana ndoto kubwa zaidi. Kutimia kwa ndoto yake kunaenda sambamba na kile kinachopigiwa chepuo kila siku na Umoja wa Mataifa kuwa uhamiaji au wahamiaji si mzigo bali ni lulu inayopaswa kulindwa kwani huleta nuru kwenye giza. Je nini kimetokea kwa mhamiaji huyu huko Nigeria? Siraj Kalyango anafafanua kwenye Makala hii.