Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nuzulack Dausen: Nishati safi inanusuru mazingira na kuinua kipato katika jamii

Nuzulack Dausen: Nishati safi inanusuru mazingira na kuinua kipato katika jamii

Pakua

Leo ni siku ya kimataifa ya nishati safi ambayo lengo lake ni kuzihimiza jamii kote duniani kutekeleza lengo la 7 la maendeleo la Umoja wa Mataifa la kuhakikisha kila mtu anahamia kwenye matumizi ya nishati hiyo ifikapo mwaka 2030. Nchini Tanzania wako msitari wa mbele katika harakati za utekelezaji wa lengo hilo na miongoni mwao ni Nuzulack Dausen mwanzilishi wa Jukwaa la kidijitali la Jiko point linaloendesha kipindi cha mwanaume jikoni kupitia mtandao wa Youtube. Amezungumza hivi karibuni jijini Dar es Salaam na Stella Vuzo afisa habari wa Umoja wa Mataifa na kumfafanulia wanavyochangia katika kufanikisha lengo la maendeleo endelevu la Umoja wa Mataifa kuhusu nishati safi. 

Audio Credit
Assumpta Massoi
Sauti
5'1"
Photo Credit
World Bank