Changamoto wanazokumbana nazo wahamiaji zaangaziwa
Vijana, wake kwa waume hukimbia makwao kutokana na usalama au kusaka maisha bora na wakati mwingi hukumbana na changamoto nyingi wakati wakitafuta hifadhi katika nchi zingine haswa zilizostawi.
Vijana, wake kwa waume hukimbia makwao kutokana na usalama au kusaka maisha bora na wakati mwingi hukumbana na changamoto nyingi wakati wakitafuta hifadhi katika nchi zingine haswa zilizostawi.
Elimu ni muhimu katika mustakhabali wa maisha ya kila mtoto na ni kwa sababu hii UNICEF inaendesha mafunzo katika familia ambazo zimejikuta katika kambi, licha ya kuwepo amani bado watu hawa wanakabiliwa na changa moto nyingi katika masiha ya kila siku basi ungana na Joseph Msami kati
Mnamo Alhamisi wiki hii, Kongamano la ngazi ya juu limefanyika huko Washington DC likiangazia vichocheo vya kijamii vinavyoweza kusaidia kutokomeza Ukimwi na umaskini uliokithiri.
Ukifikiria Umoja wa Mataifa hapana shaka unawaza juu ya jamii mbalimbali, tamaduni zao na tofuti zao zikiwa pamoja katika taasisi hii ya kimataifa. Na pia hapana shaka unawaza kuhusu masuala ya kisiasa na diplomasia ya kimataifa.
Utapiamlo ni janga la kitaifa nchini Niger na unaathiri mamia ya maelfu ya watoto.
Ni janga ,ambalo UNICEF na wadau wanajaribu kukabilina nalo kufuatia mradi bunifu wa kutoa mafunzo kwa akina mama kuweza kupima utapiamlo.
Mapigano nchini Sudan Kusini yamesababisha wimbi jipya la wakimbizi wanaowasili katika nchi jirani kutafuta usalama.
Zoezi la usaidizi kwa wapiganaji wanaojisalimisha nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC linaendelea ambapo wapiganaji hao wanajumuishwa katika jamii huku wengine wakijumuishwa katika jeshi la serikali kwa hiari.
Mwaka 2000 wakuu wa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa walipitisha malengo ya maendeleo ya Milenia, malengo yako manane na lengo namba Tatu ndiyo mada kuu ya Makala yetu wiki hii.Lengo hilo ni kuendeleza usawa wa kijinsia na kuwawezesha wanawake.