Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Habari Mpya

Bendera ya Umoja wa Mataifa ikikabidhiwa kwa maafisa wa MONUSCO nchini DRC kuashiria kufungwa kwa ofisi ndogo za ujumbe huo wa Umoja wa Mataifa wa Kulinda amani kwenye eneo hilo lililoko kilometa takribani 140 kutoka mji wa Beni jimboni Kivu Kaskazini.
UN/George Musubao

Ofisi ya MONUSCO Lubero, Kivu Kaskazini yafungwa

DRC, MONUSCO umefunga kituo chake kilichoko Lubero jimboni Kivu Kaskazini baada ya kuweko huko kwa miaka 21.Hatua hii ni sehemu ya utekelezaji wa mpango wake wa kujiondoa kwa utaratibu kutoka DRC, kwa mujibu wa azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kufuatia ombi la serikali ya DRC.

Wakiwa wamevalia mavazi ya kujikinga, daktari mwanamke anayeongoza kundi la wataalamu wa afya wanaojitolea kuhudumia wagonjwa wa COVID-19 na wanaochunguzwa katika hospitali ya jamii Ufilipino.
UN Women/Louie Pacardo

Tunahitaji kujiandaa dhidi ya janga jingine la ugonjwa: António Guterres

Janga la ugonjwa lijalo litakapotokea ni lazima tuchukue hatua kwa ufanisi zaidi kwa kuandaa na kujumuisha mafunzo tuliyojifunza kutokana na janga la COVID-19, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amesisitiza katika ujumbe wake mahususi kwa ajili ya Siku ya kimataifa ya kukabili milipuko ya magonjwa ambayo huadhimishwa kila Novemba 27 kama leo. 

Mnamo tarehe 2 Mei 2023, Hanona Yousif Mohamed Ahmed akiwa amemleta mtoto wake Maher kwenye kituo cha lishe huko Abushok, Darfur Kaskazini, Sudan kwa uchunguzi wa afya.
© UNICEF/UN0836604/Zakaria

Afya Sudan ilivyoyumbishwa na miezi 8 tu ya mzozo

Mzozo unaozidi kuwa mbaya wa Sudan unaendelea mbele ya macho yetu, ambao katika miezi 8 tu watu milioni 7 waliokimbia makazi, milioni 1.5 wamekimbilia nchi jirani, ndivyo Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa (WHO), Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus alivyoanza ujumbe wake wa kueleza namna mzozo huo umevuruga mifumo ya afya katika nchi hiyo ya kaskazini mashariki mwa Afrika.