Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Habari Mpya

Sio tu kwamba mikoko inasaidia kuzuia kuendelea kwa mabadiliko ya tabianchi, lakini pia ina jukumu muhimu katika kupunguza athari zake.
The Mangrove Photography Awards/Shyjith Kannur

Haya ndiyo mambo ya kutarajia katika Wiki ya mkutano wa Mabadiliko ya Tabianchi barani Afrika 2023

Viongozi wa Afrika wanatarajiwa kukutana jijini Nairobi, kenya wiki ijayo kwa jaili ya wiki ya mkutano wa Mabadiliko ya Tabianchi, Mkutano wa kila mwaka ambao wanatarajiwa kujadili njia mbalimbali za kupunguza utoaji wa gesi chafuzi huku wakija na mbinu za mnepo wa kukabiliana na athari za hali ya hewa.

Siku ya Kimataifa ya watu wenye asili ya Kiafrika iliadhimishwa kwa mara ya kwanza 31 Agosti 2021
PAHO

Katibu Mkuu UN ahimiza ushirikishwaji wa watu wa asili ya Afrika na jamii zao

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres kupitia ujumbe wake mahususi kwa ajili ya Siku ya Kimataifa ya Watu wa Asili ya Afrika amesisitiza tena wito wa Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa wa kutumia maadhimisho ya miaka 75 ya kupitishwa kwa Tamko la Umoja wa Mataifa la Haki za Binadamu kutangaza na kuchukua hatua haraka na madhubuti za kuendeleza usawa na kupambana na ubaguzi wa rangi, na chuki dhidi ya wageni. 

Kampuni ya Yvette Amuli, (pichani) iitwayo Buhendwa ni miongoni mwa wanufaika wa mradi wa kampuni ndogo na za kati, SME's unaoendeshwa kwa pamoja kati ya Benki ya Dunia na UN Women kwa ushirikiano na Sowers of New Hope, huko Goma, mji mkuu wa jimbo la Ki…
UN/Byobe Malenga

UN Women yainua wajasiriamali wanawake Kivu Kaskazini, DRC

Mradi wa msaada wa maendeleo ya biashara ndogo-ndogo na za kati wa Benki ya Dunia, na mshirika wake shirika la Umoja wa Mataifa la masuala ya wanawake, UN Women, umeleta manufaa katika maeneo ya mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC.  Serikali ya DRC inaeleza kuridhishwa na mradi huu ikisema kuwa umepanua kiwango cha biashara ndogo na za kati, na zaidi ya yote umeinua kiuchumi wanufaika hususan wanawake.  

Walinda amani wa Umoja wa Mataifa kutoka Tanzania kikosi cha 10, TANZBATT 10 wakiwa na wanawake wa na eneo la Mbau jimboni Kivu Kaskazini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC.
George Musubao

Msaada wenu kwetu umekuja wakati muafaka - wanawake Mbau, DRC

Mgeni njoo mwenyeji apone ni methali iliyodhihirika huko eneo la Mbau jimboni Kivu Kaskazini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC baada ya walinda amani wa Umoja wa Mataifa kutoka Tanzania kikosi cha 10, TANZBATT 10 walipotembelea hospitali ya La Grace kutoa msaada si tu wa chakula bali pia dawa. Walinda amani hawa wanahudumu kwenye kikosi cha kujibu mashambulizi, FIB cha ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo, MONUSCO.