Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Habari Mpya

Upigaji kura katika Baraza la Usalama kutengua jukumu la MINUSMA
ONU News

Baraza la Usalama kwa kauli moja limepitisha azimio kutengua jukumu la MINUSMA kuanzia leo 30 Juni 2023.

Kwa kuzingatia ombi la serikali ya mpito ya Mali la kutaka mpango wa Umoja wa Mataifa nchini humo MINUSMA uondoe mara moja na kubainisha kuwa hali ya Mali inaendelea kuwa tishio kwa amani na usalama wa kimataifa, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa leo 30 Juni limeuomba mpango wa MINUSMA kuanza mara moja tarehe 1 Julai 2023 kusitishwa kwa shughuli zake, kuhamisha majukumu yake, pamoja na uondoaji kwa utaratibu na usalama wa wafanyikazi wake, kwa madhumuni ya kukamilisha mchakato huu ifikapo tarehe 31 Desemba 2023.

Katika Makao Makuu ya UNESCO huko Paris, Ufaransa, mwonekano wa mfano wa dunia ambayo ni kazi ya kisanii ya  Erik Reitzel.
© UNESCO/Christelle ALIX

Marekani yarejeshewa uanachama wa UNESCO

Nchi 193 Wanachama wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), zilizokutana katika Mkutano Mkuu usio wa kawaida, zimeidhinisha leo Ijumaa kwa wingi sana pendekezo lililowasilishwa na Marekani la kujiunga tena na Shirika hilo ambalo walikuwa wamejiondoa mwaka 2017 chini ya Urais wa Donald Trump. 

Baadhi ya uharibifu wa mazingira na mali uliofanywa na mafuriko huko Kalehe, jimboni Kivu Kusini, DRC mwezi Mei, 2023.
UN News/George Musubao

Baada ya mafuriko Kalehe, DRC, wananchi wahamasishwa kuyalinda mazingira

Muungano wa mashirika ya kiraia katika eneo la Kalehe jimboni Kivu Kusini, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC wako katika harakati za kuhamasisha wananchi kupanda miti na kuchukua hatua nyingine zitakazosaidia kupambana na mabadiliko ya tabianchi baada ya eneo hilo kukumbwa na mafuriko yaliyosababisha vifo na uharibifu mkubwa mapema mwezi Mei Mwaka huu.

 

Sauti
4'38"
Walinda amani wa Umoja wa Mataifa wa kikosi cha sita kutoka Tanzania (TANBAT 6) wakiwafundisha mapishi wanakijiji cha Moro nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati.
TANBAT 6/Kapteni Inyoma

TANBAT6 watoa mafunzo ya mapishi na ujasiriamali kwa wanawake wanakijiji cha Moro, CAR

Walinda amani wa Umoja wa Mataifa wa kikosi cha 6 kutoka Tanzania (TANBAT 6) wanaohudumu chini ya Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Afrika ya kati, CAR (MINUSCA) wametoa mafunzo ya upishi kwa vikindi vya wanawake wa Kijiji cha Moro kilichoko takribani kilometa 50 kutoka Mji wa Berberati, jimboni Mambere Kadei yalipo makao makuu ya kikosi hicho. 

Sauti
2'11"
Wakunga wawili wakifanya kazi katika kliniki inayoungwa mkono na UNFPA nchini Sudan. (faili)
© UNFPA Sudan

Mjini Port Sudan, UNFPA inasaidia kuhakikisha uzazi salama kwa wanawake na wasichana wanaokimbia ghasia Khartoum

Wanawake  na wasichana wanaokimbia machafuko yanayoendelea mjini Kharthoum nchini Sudan wanakabiliwa na changamoto lukuki hususan kwa wajawazito wanaohitaji msaada wa kujifungua, kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu na afya ya uzazi UNFPA ambalo sasa limechukua jukumu la kuhakikisha uzazi salama kwa wanawake hao.

Sauti
2'51"
Samaki wakiogelea kuzunguka mwamba wa matumbawe katika Bahari Nyekundu karibu na pwani ya Misri.
Coral Reef Image Bank/Alexander

FAO na wadau kubeba jukumu la kuongoza mpango wa bahari safi wenye thamani ya dola milioni 115

Shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa FAO pamoja na mashirika manne wadau, wamepewa jukumu la kuongoza mpango wa pamoja wa bahari safi na zenye afya, ambao ni mradi unaolenga kuanzia kwenye chanzo taka hadi baharini  ambao utaelekeza ruzuku ya hadi dola milioni 115 kuzisaidia nchi kukabiliana na uchafuzi wa mazingira ya pwani na mfumo mzima wa Maisha ya baharí.