Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Habari Mpya

Daktari wa mifugo akimchunguza kuku mgonjwa.
FAO/Giulio Napolitano

Kutoka ukimbizi arejea nyumbani na kufuga kuku sasa ni mfano kwa wenzake Burundi

Kijana Evariste Niyonzima mkazi wa sasa wa viunga vya jiji la Bujumbura nchini Burundi aliporejea nchini mwake kutoka ukimbizini katika nchi jirani ya Tanzania, alikuwa na mawazo kuwa atakapomaliza tu masomo atapata ajira ya ofisini itakayompa kipato hadi pale alipogundua kuwa hali halisi ni tofauti na alivyofikiria. Hata hivyo hivi sasa amefanikiwa kuliko hata baadhi walioajiriwa ofisini. Alifanyaje? Edwije EMERUSENGE ni mwandishi wa Televisheni washirika, Mashariki TV ya Burundi ameipata siri ya mafaniko anasimulia zaidi.

Audio Duration
2'35"
Waandamanaji wakikusanyika mbele ya Makao Makuu ya jeshi la Sudan mjini Khartoum (11 April 2019)
Masarib/Ahmed Bahhar

Tuna hofu na ukatili wa kingono uliofanyika Sudan wakati wa maandamano- Patten

Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu ukatili wa kingono kwenye mizozo, Pramila Patten amesema ana wasiwasi mkubwa juu ya hali inayoendelea nchini Sudan kufuatia taarifa ya madai ya kuwepo kwa vitendo vya ukatili wa kingono na unyanyasaji wa kijinsia wakati wa maandamano yaliyofanyika nchini humo tarehe 19 mwezi huu wa Desemba.

Vijana nchini Mali wakishiriki kwenye maigizo kama njia mojawapo ya kupaza sauti ya amani.
MINUSMA/Marco Dormino.

Sanaa na utamaduni vyatumika kuchagiza amani nchini Mali

Tofauti zinapaswa kuimarisha jamii badala ya kuisambaratisha, huo ndio  ujumbe uliotamalaki wakati wa kampeni iliyoendeshwa nchini Mali na ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kuweka utulivu nchini humo MINUSMA kwa kushirikiana na chama cha wadau wa Umoja wa Mataifa nchini humo, MANU. Kampeni ilileta pamoja wazee kwa vijana, wanawake kwa wanaume pamoja na Watoto wenye vipaji vya Sanaa na utamaduni.

Sauti
2'39"