Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Habari Mpya

Wanafunzi jijini Dar es Salaam Tanzania wakifuatilia mafunzo kuhusu usafiri wa anga
UNIC Dar es Salaam/Ahimidiwe Olotu

Mradi wa UNESCO, UNFPA na UN Women wapokelewa vizuri ndani ya jamii nchini Tanzania 

Wazazi nchini Tanzania wameupokea vizuri mradi unaotekelezwa na mashirika matatu ya Umoja wa Mataifa, lile la elimu, sayansi na utamaduni, UNESCO, la masuala ya idadi ya UNFPA na la wanawake UN Women, ambao unalenga kuwawezesha wasichana kupitia elimu. Baada ya jana kuwaangazia wasichana wanufaika wa mradi huu, leo, Ahimidiwe Olotu ametuandalia sehemu ya pili inayoangazia wazazi na wanajamii kwa ujumla.   

Sauti
2'38"
Boto ilizama pwani ya Libya ikiripotiwa kubeba zaidi ya watu 120 na kati yao ni 47 tu walinusurika kifo.
IOM/Hussein Ben Mosa

Chondechonde tuwanusuru wakimbizi na wahamiaji wanaolazimika kuvuka Mediterrania:UNHCR 

Wakati zahma zikiongezeka Afrika Kusini mwa jangwa la Sahara na kuwalazimisha mamilioni ya watu kufungasha virago, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limetoa raia ya kuongeza juhudi za kuwasaidia wakimbizi na wahamiaji hasa wanaobidi kupitia njia hatari kwenye bahari ya Mediterrania kwenda kusaka mustakbali bora.

Sauti
2'36"