Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Habari Mpya

Tembo yatima aliyeokolewa huko David Sheldrick kituo cha  Wanyamapori Trust nchini Kenya.
UNEP/Natalia Mroz

Kutoka kuwa adui wa tembo hadi rafiki na mtetezi- Edwin Kinyanjui 

Nchini Kenya kampeni ya kulinda wanyamapori nayoongozwa na shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa, UNEP imezidi kupanua wigo wake ambapo hivi sasa hata watu ambao awali walikuwa adui wa wanyamapori, wamegeuka rafiki na walinzi wakuu wa wanyama hao kama njia mojawapo ya kuhifadhi misitu kama ile ya mlima  Kenya, bali pia bayonuai ambayo ni muhimu kwa viumbe vyote.

Sauti
2'20"
Haya Ali akiwa na mwanae wa miezi sita akiwa kwenye makazai ya jamii yanayoendeshwa na UNHCR, Tripoli, Libya. Anatokea Asmara, Eritrea.
UN OCHA/GILES CLARKE

Huduma kwa wajawazito Libya zinazowezeshwa na UNHCR mkombozi wa wakimbizi wa Eritrea

Kama sehemu ya huduma mbali mbali za ulinzi zinazotolewa kwa wakimbizi na wanaotafuta hifadhi nchini Libya, shirika la kuhudumia wakimbizi UNHCR kupitia mdau wake, Kamati ya kimataifa ya uokozi, IRC, wanatoa huduma za afya ya uzazi bila malipo kwa wanawake ambao ni wajawazito au wamejifungua hivi karibuni, na pia kuwapatia rufaa za kwenda kwenye vituo vikubwa zaidi kwa ajili ya kujifungua.

Sauti
2'13"
Familia iliyokimbia makazi yao, wakiwa katika hema la muda katika kambi kaskazini mwa vijijini Aleppo, Syria.
© UNICEF/Ali Almatar

Wasyria 9 kati ya 10 wanaishi kwenye umaskini, tuwasaidie – Guterres

Kupitia katika ujumbe wa video kwa Mkutano wa tano unaofanyika Brussels, Ubelgiji,  kuunga mkono Syria na ukanda huo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametoa wito kwa wafadhili kusaidia kushughulikia mahitaji yanayoongezeka na kuongeza ahadi za kifedha na kibinadamu kuwasaidia Wasyria na "kupunguza mzigo mkubwa wa kifedha wa nchi ambazo zinahifadhi wakimbizi.” 

Mwanamke akichuuza mbogamboga nchini Gambia.
FAO/Seyllou Diallo

Msaada wa IFAD umeniokoa mimi na familia yangu: Mjasiriamali Fatou 

Duniani kote mamilioni ya wasichana na wanawake vijijini wanaweza kuendesha maisha yao kwa kutumia ardhi inayowazunguka, lakini mara nyingi wanashindwa kufanya hivyo kwa ukosefu wa mtaji wa kuanzia kutekeleza malengo yao, Sasa mfuko wa kimataifa wa maendeleo ya kilimo IFAD unashirikiana na serikali mbalimbali kutoa mitaji inayowawezesha wasichana kuingia katika bishara ya kilimo kama  alivyofanya Fatou Secan nchini Gambia.

Sauti
2'3"