Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Habari Mpya

Vipimo vya virusi vya ukimwi.
Public Health Alliance/Ukraine

Vipimo vya VVU vyapungua UNITAID waomba ufadhili zaidi

Kuelekea kilele cha siku ya UKIMWI Duniani Desemba 1, Shirika la Umoja wa Mataifa la kufanikisha upatikanaji wa dawa za tiba kwa gharama nafuu, UNITAID limesema usumbufu na ucheleweshaji wa huduma za VVU unaosababishwa na janga la COVID-19 ulisababisha kupungua kwa vifaa vya upimaji na utambuzi wa VVU kwa kiwango kikubwa ambacho hakijawahi kuonekana ndani ya miongo miwili.

Sauti
2'28"
Chanzo zilizotolewa kwa Tanzania kwa msaada wa Marekani kupitia mpango wa Umoja wa Mataifa wa kusaka chanjo za Corona au COVID-19, COVAX, na ziliwasili tarehe 24 Julai 2021.
UNICEF/Daniel Msirikale

AU yatoa masharti 6 kwa wanaotoa msaada wa chanjo za COVID-19 Afrika

Kuanzia Januari mosi mwaka 2022 kama kuna nchi au shirika la kimataifa linataka kutoa msaada wa chanjo za Corona au COVID-19 barani Afrika, basi linapaswa kufuata masharti kadhaa yaliyotolewa leo na Muungano wa Afrika AU kwa kushirikiana na mashirika mengine tanzu kama vile kituo cha Afrika cha kudhibiti magonjwa CDC na GAVI COVAX  na AVAT yenye jukumu kuu la uwakala  mkuu wa ununuzi kwa niaba ya AU.

Lucy Adjeley Boye, mmoja wa wanufaika wa mradi wa Benki ya Dunia wa ujenzi wa vyoo imara na salama kwenye mji mkuu wa Ghana, Accra
Video Benki ya Dunia

Kujisaidia kwenye vifuko vya nailoni kumebakia historia- Mkazi wa Accra

Nchini Ghana, huko Afrika Magharibi ukosefu wa choo umekuwa ni adha kubwa kwa wakazi wa kitongoji kimoja maarufu kwa utalii kwenye mji mkuu Accra. Vifuko vya nailoni vilivyosheheni haja kubwa vilikuwa ni jambo la kawaida hadi Benki ya Dunia ilipoingilia kati na kusaidia mamlaka ya majisafi na majitaka ya jiij la Accra, GAMA. Sasa kuna ahueni na wananchi wamefunguka macho.

 

Mtoa huduma ya afya nchini Mali akijiandaa kutoa chanjo ya COVID-19 , jumla ya chanjo 396,000 zimesambazwa Afrika Magharibi na COVAX
© UNICEF/Seyba Keïta

WHO inasimama na mataifa ya Afrika, chonde chonde msifunge mipaka

Wakati idadi ya nchi zinazotangaza marufuku ya safari za ndege kwa mataifa ya Kusini mwa Afrika ikiongezeka kutokana na hofu ya aina mpya ya virusi vya COVID-19 vya Omicron, shirika la afya la Umoja wa Mataifa ulimwenguni WHO leo limezisihi nchi kufuata sayansi na kanuni za kimataifa za afya za mwaka 2005.