Idadi ya wanaume wanaotumia bidhaa za tumbaku imepungua- Ripoti, WHO
Shirika la afya ulimwenguni, WHO linakadiria kwa mara ya kwanza kwamba idadi ya wanaume wanaotumia tumbaku imepungua ikiashiria mabadliko katika janga la tumbaku kimataifa.
Shirika la afya ulimwenguni, WHO linakadiria kwa mara ya kwanza kwamba idadi ya wanaume wanaotumia tumbaku imepungua ikiashiria mabadliko katika janga la tumbaku kimataifa.
Wanafunzi kote nchini Sudan Kusini wakiwemo wale wanaoishi katika vituo vya Umoja wa Usalama vya kuwahakikishia raia usalama, wanafanya mitihani ya mwisho wa mwaka ambapo mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, UNMISS inafanya kazi ya kuwapeleka wanafunzi wa kambini katika shule wanakofanyia mitihani na pia kuwarejesha.
Mkutano wa kwanza wa ngazi ya juu kuhusu wakimbizi umefunga pazia huko Geneva, Uswisi ukiwa na ahadi lukuki za kusaidia wakimbizi na jamii zinazowahifadhi huku ahadi nyingi zaidi zikijikita katika usaidizi wa muda mrefu hususan ujumuishaji.
Hatimaye nuru imeangazia wagonjwa wa saratani ya titi husasan katika nchi za kipato cha chini baada ya shirika la afya duniani WHO hii leo kuidhinisha kutengenezwa kwa dawa ya mfanano ya gharama nafuu iitwayo TRASTUZUMAB.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa pamoja na viongozi wengine wa juu wa Umoja wa Mataifa, wametoa wito kwa dunia kuhakikishia ulinzi wa haki za binadamu kwa wahamiaji.
Maandamano yanayoshuhudiwa hivi sasa katika kila kona ya dunia ni kumbusho kwamba sauti za watoto na barubaru zinapaswa kusikika na haki zao kulindwa amesema mkurugenzi mtendaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa pamoja na viongozi wengine wa juu wa Umoja wa Mataifa, wakitoa wito kwa dunia kuhakikishia ulinzi wa haki za binadamu kwa wahamiaji. Asya Omar Mwilima ni mhamiaji kutoka Zanzibar Tanzania ambaye alihamia nchini Marekani takribani miaka 20 iliyopita na anakubaliana na wito wa Umoja wa Mataifa.
Somalia ikielekea wakati muhimu katika mustakabali wa amani ya taifa hilo lililokuwa kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe kwa zaidi ya miongo mwili sasa, imeaswa na Umoja wa Mataifa kuonyesha mshikamano katika malengo iliyojiwekea 2020.
Nchi zinastahili kuzipa haki za binadamua umuhimu katika sera zao na mijadala inayohusu uhamiaji na kuchukua hatua za kumaliza kauli za uchochezi, kwa mujibu wa wataalamu wa haki za binadamu wa umoja wa Mataifa kwenye ujumbe wao kuelekea siku ya uhamiaji duniani tarehe 18 Desemba.
Lugha za asili bado ni muhimu kwa mustakabali wa ulimwengu hivyo tufanye kila namna kuzitunza, ni moja ya kauli alizozitoa rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Tijjani Muhammad Bande katika mkutano wa ngazi za juu wa kuhitimisha mwaka wa kimataifa wa lugha za asili uliofanyika hii leo katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York Marekani.