Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kabrasha la Sauti

08 DESEMBA 2023

Hii leo kwenye jarida Assumpta Massoi anamulika mzozo Mashariki ya Kati hususan huko Gaza,  nyaya za simu zageuzwa kuni, kisha anakwenda Mashariki mwa Afrika huko baada ya ukame wa muda mrefu sasa ni mvua za kupindukia zinazosababisha maafa makubwa,; makala anakupeleka Tanzania kusikia ucham

Sauti
9'45"
Habari za UN

NENO: Kifandugu

Leo katika Jifunze Kiswahili ukumbi ni wake mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa  nchini Tanzania , BAKITA anafafanua maana ya neno “KIFANDUGU”.  Anapochambua neno hili anapatia pia kisawe chake ambacho ni "KITOKONO."

Sauti
59"

07 DESEMBA 2023

Hii leo kwenye jarida Leah Mushi anakuletea Habari kwa Ufupi ikiangazia Tanzania, janga la chakula Afrika na Mkutano wa UN na wanazuoni. Katika Mada kwa Kina tunamulika mshindi wa Tuzo ya UN ya Haki za Binadamu Julienne Lusenge kutoka DRC na Jifunze Kiswahili maana ya neno, Kifandugu.

Sauti
11'41"
©UNICEF/UNI472270/Zaqout

Uchunguzi ufanywe Gaza kuhusu madai ya ukatili wa kingono wakati wa shambulio la Hamas - OHCHR

Kamishina Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Volker Türk leo amelaani vikali ukiukaji mkubwa wa haki wa kingono dhidi ya Waisraeli unaodaiwa kutekelezwa na wanamgambo wa Hamas wakati wa mashambulizi yao ya kigaidi kusini mwa Israel tarehe 7 Oktoba, huku wahudumu wa kibinadamu huko Gaza

Audio Duration
1'53"