Wanawake wanaajirika, wanaweza: Sophia Simba
Wanawake wanaajirika, wamesoma na wamepewa nafasi za uongozi, ni kauli ya matumaini ya waziri wa maendeleo ya jamii, jinsia na watoto wa Tanzania Sophia Simba wakati wa mahojiano na Joseph Msami muda mfupi baada y akuhudhuria mkutano kuhusu usawa wa kijinsia mjini New York.