Watu wenye ulemavu mashinani kuhudumiwa Tanzania
Wananchi mkoani Kagera nchini Tanzania watanufaika na huduma zitolewazo kwa watu wenye ulemavu baad ya ya kituo cha kuhudumia makundi hayo wilayani Karagwe kuanza kufanya kazi.
Wananchi mkoani Kagera nchini Tanzania watanufaika na huduma zitolewazo kwa watu wenye ulemavu baad ya ya kituo cha kuhudumia makundi hayo wilayani Karagwe kuanza kufanya kazi.
Maji ni uhai!
Utamaduni ambao huchukua sehemu kubwa ya maisha huhusisha pia ngoma au muziki mbalimbali ambazo hutumiwa na jamii kwa malengo kadhaa ikiwamo kuwaleta pamoja wanajamii wa makundi tofauti, burudani na hata wakati wa matukio maalum ya jamii husika.
Mila potofu zinazokandamiza wanawake ni moja ya sababau zinazozuia maendeleo endelevu katika nchi zinazoendelea kwani hupokonya haki za wanawake na kurudisha nyuma kimaendelo.
Licha ya kwamba nchi nyingi zimepitisha sera ya matibabu ya bure kwa wazee, huduma hiyo imekuwa ni changamoto kubwa hususani barani Afrika ambapo wengi wa wazee hutaabika wakati wa kusaka huduma za afya.
Siku ya kimataifa ya vijana ambayo huadhimishwa kila Agosti 12 hulenga kuangalia ustwawi wa kundi hilo katika nyanja ya kijamii, kiuchumi, masuala ya elimu, afya na mengineyo.Mwaka huu maudhui ni ushiriki wa vijana katika masuala ya kisiasa.
Kutokana na huduma za elimu zisizoridhisha wazazi na wanafunzi katika kambi za wakimbizi nchini Uganda, wazazi huhaha kuwapeleka watoto wao katika shule za mijini.
Tuwashemu na kuwapa kipaumbele watoa misaada kwani wanafanya kazi nyeti katika maeneo yenye majanga. Amesema mtaalamu mweza wa menejimenti ya mpango katika ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya kibinadamu OCHA, Sarah Oseombo.
Migogoro imeendelea kusababisha wimbi kubwa la wakimbizi na wahamiaji wanaosaka hifadhi. Raia hawa wasIo na hatia hukumbana na kadhia kadhaa wakati wa kusaka hifadhi ikiwamo kuhatarisha usalama wao na jamaa zao na hata afya zao.
Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO kupitia mradi wake, "Kuimarisha Radio za kijamii kutumia teknohama”, linatoa mafunzo kwa redio 32 katika nchi saba barani Afrika.