Makala yenye kuangazia siku ya urafiki duniani
Tarehe 30 Julai, jamii ya kimataifa imeadhimisha siku ya urafiki duniani, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa akisema urafiki hujenga daraja baina ya watu, na hivyo huchochea amani duniani.
Tarehe 30 Julai, jamii ya kimataifa imeadhimisha siku ya urafiki duniani, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa akisema urafiki hujenga daraja baina ya watu, na hivyo huchochea amani duniani.
Ikiwa leo ni Siku ya Kimataifa ya Urafiki, inayotumiwa na Umoja wa Mataifa kujenga urafiki na kuunganisha jamii kwa ajili ya amani na ustawi, nchini Uganda raia wa nchi hiyo wanaeleza kwao urafiki una maana gani .
Klabu ya Uhispania ya soka FC Barcelona imo katika ziara ya Amerika Kaskazini, kabla ya msimu mpya wa soka kuanza mnamo mwezi Agosti.
Takriban vijana milioni 74 walikuwa wanasaka ajira mwaka 2014! Hii ni kulingana na ripoti ya Shirika la kazi duniani ILO.
Mti wa Calliandra sasa ni mtaji kwa wakulima, wafugaji na hata katika kutunza mazingira wakati huu ambapo dunia ina kilio cha mabadiliko ya tabia nchi.
Ungana na John Kibego kutoka Uganda kwa makala kuhusu mti huo na manufaa yake kwa makundi hayo na kwa jamii nzima kwa ujumla.
Usafi wa mazingira jijini Mwanza Tanzania sio tu kwamba umewezesha muoneakano bora wa jiji hilo, bali pia umeinua kipato cha wanavikundi ambao wamelivalia njuga suala la usafi katika maeneo mbalimbali ya jiji hilo.
Kongamano la tatu la kimataifa kuhusu ufadhili kwa maendeleo limefanyika mjini Addis Ababa, Ethiopia, kuanzia Jumatatu tarehe 13 hadi Alhamis tarehe kumi na sita wiki hii.
Leo ikiwa ni siku ya kimataifa ya ujuzi kwa vijana inashangaza kuona kuwa baadhi ya vijana wanajishughulisha katika kujikwamua kiuchumi lakini wengi hawafahamu kuhusu malengo ya maendelo ya milenia amesema mbunge kijana kutoka Tanzania Ridhiwani Kikiwete.
Wakati malengo ya maendeleo ya milenia MDGS yakifikia ukomo mwezi Septemba mwaka huu, nchi kadhaa zimejitahidi kutimiza malengo hayo manane likiwemo lengo namba mbili la kukuza elimu ya msingi kwa wote ambapo nchini Uganda serikali kwa kushirikiana na wadau imepiga hatua.
Nchi wanachama za Umoja wa Mataifa zikikutana mjini Addis Ababa nchini Ethiopia kwa ajili ya kongamano la kimataifa kuhusu Ufadhili kwa Maendeleo, mashirika yasiyo ya kiserikali yamekuwa na mkutano maalum mwishoni mwa juma .