Nishati ya samadi ya wanayama yabadili maisha ya wanavijiji Nepal
Matumizi ya nishati ya kupikia inayotunza na kuhifadhi mazingira imeleta mwanga kwa jamii nchini Nepal hususani maeneo ya vijijini.
Matumizi ya nishati ya kupikia inayotunza na kuhifadhi mazingira imeleta mwanga kwa jamii nchini Nepal hususani maeneo ya vijijini.
Mapema wiki hii nchini Kenya, kumefanyika warsha kwa ajili ya kuimarisha upatikanji wa vifaa vya kujifunzia na kufundishia, OER, kwa lengo la kuimarisha elimu barani Afrika. Warsha hiyo iliendeshwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu Sayansi na Utamaduni, UNESCO mjini Nairobi Kenya.
Hatimaye pazia la mkutano wa masafa ya radio limefungwa huko Geneva, Uswisi baada ya takribani mwezi mmoja wa majadiliano kuhusu masafa hayo kwa maslahi ya wakazi wa dunia hii.
Makundi yenye msimamo mkali na ugaidi ni tishio kubwa kwa amani na usalama duniani. Nchi na mashirika mbalimbali yanasaka suluhu ya kimataifa kwa janga hili linalokuwa kwa kasi na kuathiri jamii katika nyanja mbalimbali ikiwamo kijamii, kiuchumi na hata kiutamaduni.]
Vijana na watoto kutoka Marekani na Indonesia wanajiandaa kwenda Paris, nchini Ufaransa, kuhudhuria kongamano la kimataifa kuhusu tabianchi kati ya Novemba 30 na Disemba 11 mwaka huu, baada ya kushinda shindano la vijana la muziki kuhusu changamoto za dunia.
Nchini Kenya, msongamano wa magari ikiwemo yale ya binafsi na ya umma, umekuwa ni mwiba kwa wasafiri hususan kwenye mji mkuu Nairobi na viunga vyake. Msongamano huo husababisha watu siyo tu kuchelewa makazini, bali pia rabsha za hapa na pale kati ya watoa huduma na wahudumiwa.
Kwa kutambua umuhimu wa kulinda mazingira kufuatia mikakati mbali mbali ambayo dunia imechukua kwa ajili ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, wananchi na watu wenye ushawishi katika jamii wanashiriki katika kuhamasisha umma kuhusu ulinzi wa mazingira.
Kila siku, maelfu ya wakimbizi na wahamiaji wanaweka maisha yao hatarini katika safari ya kuvuka bahari ya Mediteranea, wengi wao wakikimbia mateso na hali ngumu za maisha. Idadi kubwa wanatoka Syria, Iraq na Afghanistan wakipitia Ugiriki ili kufika nchi nyingine za Ulaya.
Lengo namba moja la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs yaliyopitishwa mwezi Septemba mwaka huu linataka umaskini uwe umetokomezwa ifikapo mwaka 2030.
Makubaliano yamefikiwa na mkutano mkuu wa masafa ya radio kwa ajili ya kutenga masafa maalumu ya kufuatilia ndege popote pale ikiwemo katika maeneo ya juu ya maji.