Miaka 70 ya UM Tanzania, yapo mengi ya kujivunia:
Mwaka 1945 Umoja wa Mataifa ulianzishwa kwa malengo mahsusi ikiwemo kuendeleza amani na usalama duniani, kuchagiza maendeleo endelevu na kutetea haki za binadamu.
Mwaka 1945 Umoja wa Mataifa ulianzishwa kwa malengo mahsusi ikiwemo kuendeleza amani na usalama duniani, kuchagiza maendeleo endelevu na kutetea haki za binadamu.
Hali ya kibinadamu nchini Yemen inazidi kuzorota kwa kasi, na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR inatarajia kuwa katika miezi michache ijayo zaidi ya wakimbizi 30,000 kutoka Yemen watawasili pwani ya Djibouti na wengine 100,000 nchi jirani ya Somalia.
Katika kukabiliana na malaria nchini Kenya mbinu mbadala zimekuwa zikitumika mathalani utafiti na mbinu shirikishi ili kutimiza lengo la kuwa na jamii isiyo na maambukizi ya malaria ugonjwa unaosababishwa na mbu aina ya anophlex ambako takwimu za mwaka jana zinaashiria kwamba takriban watu milion
Vijana wa kimaasai huathirka sana kwa kukosa kazi na wanatumbukia katika majanga kama vile kuuza madawa ya kulevya, ni kauli ya mwakilishi wa jamai ya kimasaai kutoka Tanzania aliye pia mwakilishi wa shirika la maendeleo ya wanawakwe wamaasai MWEDO, Ndinini Kimesirasika.
Katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa wiki hii kumefanyika mjadala kuhusu stahamala na maelewano baina ya watu wa imani tofauti za kidini.
Dunia ikiwa inashuhudia matukio ya kigaidi na machafuko yanyotokana na chuki sehemu mbalimbali, makundi yanayojihusisha na ugaidi na machafuko mengine yamekuwa yakitumia mwavuli wa dini katika kuhasisha na hata kutekeleza mashambulizi.
Baada ya kadhia ya mlipuko wa ugonjwa wa Ebola uliosababisha vifo ya maelfu ya watu, katika nchi za Afrika ya Magharibi hususan Liberia, Sierra Leone na Guinea, shule ambazo zilifungwa awali ili kuepuka maambukizi zaidi zimefunguliwa.
Zaidi ya asilimia 93 ya watanzania wanaishi kwenye maeneo ambayo yanawaweka hatarini kukumbwa na Malaria. Hata hivyo serikali ya Tanzania imekuwa mstari wa mbele kuchukua hatua za kinga, tiba na utambuzi wa mapema ili kudhibiti kuenea kwa Malaria.
Mwakilishi wa asasi ya kiraia kutoka Kenya iitwayo mtandao wa barubaru na vijana Afrika, NAYA kwa upande wa Kenya Robert Aseda amesema kabla ya kusubiri uwezeshaji kutoka nje shirika hilo linatumia ujuzi wa vijana mbalimbali kwa kuwaimarisha.
Mkutano wa 48 kuhusu idadi ya watu na maendeleo ulioandaliwa na tume ya idadi na maendeleo CPD umekamilika leo hapa New York . Makundi mablaimbai ya wadau wa maendelo wamejadili namana wanavyoweza kukuza maendeleo kwa kuzingtia ajenda ya maendeleo baada ya mwaka 2015.