Burundi ikielekea uchaguzi mkuu , Umoja wa Mataifa wataka utulivu
Taifa la Burundi lilioko Afrika Mashariki , linajiandaa kwa uchaguzi mkuu mwezi mei mwaka huu. Hata hivyo joto la kisiasa limeanza kupanda miezi mitatu kabla ya zoezi hilo.
Taifa la Burundi lilioko Afrika Mashariki , linajiandaa kwa uchaguzi mkuu mwezi mei mwaka huu. Hata hivyo joto la kisiasa limeanza kupanda miezi mitatu kabla ya zoezi hilo.
Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, mzozo Mashariki mwa nchi hiyo umetumbukiza watoto na vijana katika kutumikishwa vitani. Hata hivyo shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF linahaha kila uchao kuwanasua watoto hao kutoka mikono ya watumikishaji.
Watu wenye ulemavu wanoishi katika jamii zisizo na mazingira mujarabu kwa kundi hilo, hukumbana na madhila kadhaa.
Meja Jenerali Leonard Ngondi amemaliza muda wake kama mkuu wa vikosi vya Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Liberia UNMIL.
Miezi minne baada ya kuaga dunia jijini New York, Marekani, Hayati Profesa Ali Mazrui msomi na nguli wa fasihi kutoka Kenya amefanyiwa hafla maalum kwenye Umoja wa Mataifa jijini New York kutokana na mchango wake kwenye shughuli za Umoja huo.
Baada ya visa 25 vya Ebola kuibuka kwenye kijiji cha Aberdeen, nchini Sierra Leone, kijiji kizima kimewekwa kwenye karantini.
Nchini Ukraine, mapigano yanayoendelea mashariki mwa nchi hiyo yameacha wananchi wengi katika dimbwi la sintofahamu, wakihaha kutwa kucha kusaka hifadhi.
Hifadhi ya bayoanuai iliyopo baharini ni changamoto kubwa hasa wakati ambapo asilimia 64 ya maeneo ya bahari hayamilikiwi na nchi yoyote.
Tarehe 21 mwezi Februari kila mwaka ni siku ya lugha ya mama duniani! Lengo ni kuhamasisha matumizi ya lugha ya mama katika nyanja mbali mbali ikiwemo kielimu.
Umuhimu wa redio katika jamii mbalimbali ni dhahiri ikizingatiwa kwamba chombo hiki kinatumika kwa mawasiliano na maswala mbalimbali ya kijamii. Pia redio ni daraja ya mawasiliano kati ya wananchi na serikali, hususan katika maeneo ya pembezoni.