“Dharura ya tabianchi ni changamoto inayotushinda, lakini tuna uwezo wa kushinda”, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ameuambia mkutano huo.
Siku ya Jumamosi, vijana walifanya mkutano wao wenyewe kwenye Umoja wa Mataifa ili kuonyesha hisia zao kuhusu ongezeko la haraka la joto duniani . Hapa, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, akizungumza na mcheza filamu kijana Aidan Gallagher, Balozi Mwema wa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP)
Viongozi wa ulimwengu watakutana Jumaane wiki hii ili kujadili Malengo ya Maendeleo Endelevu - malengo 17 ya kupunguza umasikini duniani na kusongesha maendeleo endelevu na maendeleo yenye usawa. Pia, kuna mkutano wa ngazi ya juu unaohusu nchi za visiwa vidogo vinavyoendelea, kwa kuzingatia changamoto za kipekee zinazokumba visiwa hivyo, huku vina vya bahari vikiongezeka kote ulimwenguni.
Mwanaharakati wa mabadiliko ya tabianchi anayetoka Uswis, Greta Thunberg (kulia) akiwa pichani na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres (kushoto) akihudhuria Mkutano wa Hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi wenye lengo la kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
Siku ya Jumamosi, vijana walikusanyika kwenye mkutano mkutano wao wa Umoja wa Mataifa wa tabianchi uliofanyika kwa mara ya kwanza. Mcheza filamu kijana na Balozi Mwema wa shirika la mpango wa Mazingira la Umoja wa Mataifa UNEP, Balozi Aidan Gallagher (aliyekaa kulia), akipitia hotuba yake kabla ya kuhutubia mkutano huo.
Mwakilishi maalum wa vijana wa Umoja wa Mataifa Jayathma Wickramanayake aligusia suala la maandano ya vijana dunia nzima dhidi ya harakati za kupambana na mabadiliko ya tabianchi na akasema kwamba ujumbe kwa watu wazima uko wazi.
“Vijana wanahitaji mchukue hatua ili tuwe na mustakabali mzuri, ili tuwe na sayari ambayo ni makazi mazuri ya kuishi”.