Walinda amani wapatao 88,000 hivi sasa wanahudumu maeneo mbalimbali duniani chini ya bendera ya Umoja wa Mataifa katika jumbe mbalimbali za ulinzi wa amani. Kulinda raia wakati wa migogoro, kwa mfano (kama ilivyo pichani ambapo nchini Mali), ni sehemu muhimu ya mamlaka yao.
Doria ya walinda amani wa Umoja wa Mataifa katika maeneo yenye migogoro, kama inavyoonekana pichani ambako ni Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC, husaidia kuimarisha usalama, kulinda raia kutoshambuliwa na kuongeza imani ya wakazi wa eneo hilo
Walinda amani pia wanalinda misafara ya watoa misaada ya kibinadamu kwenye maeneo yaliyoathiriwa na migogoro. Mathalani nchini Sudan Kusini ambako shirika la mpango wa chakula duniani, WFP, linaangusha shehena za chakula kutoka kwenye ndege zao angani kwa watu walioko katika mazingira magumu.
Tangu mwaka 1948, zaidi ya watu milioni moja wanaume na wanawake wamehudumu katika opereshani za ulinzi wa amani za Umoja wa Mataifa. Pichani, ni afisa polisi wa Umoja wa Mataifa katika ujumbe wa kulinda amani huko nchini Lebanon, (UNFIL) akizungumza na raia mkazi wa eneo hilo
Walinda amani hufanya kazi pamoja na wenzao ambao ni wahudumu wa misaada ya kibinadamu. Pichani ni mlinda amani kutoka Misri anayehudumu kwenye ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kuweka utulivu nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR, akimsaidia raia kuteka maji kwenye kisima ambacho kimejengwa kwa ufadhili wa MINUSCA.
Walinda amani wa Umoja wa Mataifa si wanajeshi na polisi wanaofanya kazi kwenye jumbe za ulinzi wa amani za Umoja wa Mataifa bali pia kuna wafanyakazi 14,000 raia ambao hufanya kazi chini ya bendera ya buluu ya Umoja wa Mataifa. Miongoni mwa hao raia ni zaidi ya wafanyakazi 600 wanaohusika na masuala ya haki za binadamu wakihudumu katika jumbe tisa. Pichani ni nchini Sudan Kusini ambako wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa wana mamlaka ya kufuatilia na kuchunguza ukiukwaji wa haki za binadamu.