Hali ya kibinadamu inaimarika ingawa bado inayumba
Wakati mafuriko yalikumba nchi hiyo mwaka 2016 na kusomba nyumba yake Julienne hakuwa na chaguo bali kuondoka nymbani kwake na kwenda kusaka hifadhi kwenye kambi ya Gitaza katika jimbo la Rumonge akiwa na watoto wake wanane kwa muda wa miaka miwili. “Tuliishi katika mazingira ya umasikini sana nadni ya hema lililochanika na dogo kama kiota cha ndege na watoto wanane , hali ilikuwa ngumu sana” Hata hivyo shukrani ziwaendee washirika wa ufadhili na serikali ya Burundikwani Julienne na wanawe walipatiwa msaada wa malazi na fecha za kujenga upya maisha yao.
Hapo awali wakiwa wakimbizi nchini Tanzania, familia hii iliamua kurejea Burundi Aprili 2018. Katika kambi ya muda ya Mabanda jimbo la Makamba ambako walipatiwa msaada wa kibibnadamu kabla ya ya kusafirishwa kwenda kwenye maeneo waliyotoka, walielezea furaha yao ya hatimaye wamefanikiwa kurejea nyumbani.
Kutokuwa na uhakika wa chakula na Utapiamlo
Wakati chakula la mapato ya kilimo yalipoongezeka mwaka 2018 , bado uhakika wa chakula umesalia kuwa changamoto nchini Burundi ukiathiri watu milioni 1.72. Wakulima vijijini wanakabiliwa na mmomonyoko wa udongo , shinikizo katika rasilimali ,upungufu wa zana za kilimo, kutokea kwa majanga ya asili mara kwa mara na wadudu waharibifu wa mimea wanaoathiri mavuno.
Uwiano wa idadi ya watu wa Burundi ni wa pili wa kiwango cha juu zaidi katika bara la Afrika, ambao unaongeza shinikizo la ziada kwenye rasilimali ambazo tayari ni haba nchini humo.
Jacqueline anaishi na watoto wake sita kwenye jimbo la Kirundo. Ni mkulima lakini hakuweza kuvuna chochote mwanzoni mwa mwaka kutokana na uhaba wa mvua mwezi Novemba ambao ndio msimu wa masika. Mavuno ya miaka mitatu mfululizo yamepotea kutokana na ukame na hivyo kumuweka yeye na familia yake katika hali mbaya.. Mara nyingi Jacqueline anaweza kuipa familia yake mlo mmoja tu kwa siku . Tayari ameshauza ng’ombe wake ili kununua chakuka sokoni ambako bei imepanda mara mbili kutokana na ongezeko la wahitaji. Mmoja wa watoto wake anasumbuliwa na utapiamlo , lakini hawezi kumudu usafiri wa kumpeleka katika kituo cha jirani cha afya.
Mabadiliko ya tabia nchi athari zinajirudia na kuathiri mnepo
Yakisambaratisha nyumba na mazao , majanga ya asili ni chanzo kikuu wakimbizi wa ndani nchini Buriundi. Robo tatu ya wakimbizi wote wa ndani ambao ni 130,000 ni kutokana na athari za mabadiliko ya tabianchi. Mwaka 2018 mvua kubwa na upepo mkali viliwaathiri takriban watu 100,000 na kuwatawanya asilimia 20 ya idadi hiyo.
Kufuatia mvua hizo , mjini Bujumbura Elizabeth na mumewe , wazazi wake na watoto wake saba walipoteza kila kitu, na nyumba yao ya matofali ya matope iliporomoka na kila kitu chao kusombwa na mafuriko ikiwemo akiba ya chakula cha familia
Watu kuhamahama kunaendelea kuongeza mahitaji ya kibinadamu
Zaidi ya asilimia 50 ya wakimbizi wa ndani na zaidi ya theluthi moja ya wakimbizi wa Burundi wanaorejea nyumbani wanahifadhiwa na jamii za waburundi wenyewe na hivyo kuongeza shinikizo katika rasilimali ambazo tayari ni adimu na wakati mwingine kusababisha migogoro ya ardhi. Shukran kwa sera ya serikali ya kufungua milango na ukarimu kwamba pia kuna wakimbizi wengine 76,000 kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, wanaoishi nchini Burundi na ambao wanaendelea kuhitaji msaada.
Wakati wa ziara yake rasmi nchini Burundi Septemba 2018, Msaidizi wa Katibu mkuu wa masuala ya kibinadamu na naibu mratibu wa OCHA Bi. Ursula Mueller, alitembelea kituo cha muda cha Songore kwenye jimbo la Ngozi . Na aliguswa sana na maekezo ya Beatrice na Emmanuel, ambao walirejea Burundi baada ya kuishi ukimbizini Tanzabnia kwa miaka miwili wakitarajia kuwa na maisha bora na mapya nchini mwao.
Kuna hatari kubwa ya milipuko ya maradhi
Mara kwa mara katika majimbo ya mpakani na ziwa Tanganyika , kipindupindu na magonjwa ya kuhara yanaongezeka kutokana na ukosefu wa maji safi na salama ya kunywa na hali ya usafi. Mvua kubwa zinachangia mazingira haya machafu kutokana na vyoo kufurika. Pia ongezoko la mbu zlinaongeza hatari ya milipuko ya malaria.
Kwa mujibu wa shirika la afya ulimwenguni WHO kumekuwa na hofu ya ongezeko la malaria Burundi tangu mwezi Novemba mwaka jana. Na visa milioni 1.85 vipya vya malaria vimeripotiwa katika miezi mitatu ya mwanzo ya mwaka 2019 ikiwa ni ongezeko la asilimia 36 ikilinganishwa na wakati kama huo 2018.