Julai 17 ni Siku ya kimataifa ya Haki dhidi ya Uhalifu. Katika makao makuu ya UN jijini New York, Marekani maonesho ya picha yanadhihirisha jinsi mizozo inavyosambaratisha jamii na jinsi msaada wa ujenzi mpya unaotolewa na wanajamii ndani ya eneo hilo hilo unavyoleta mabadiliko makubwa kwenye maisha.
Aicha, mkuu wa Nessemon, hiki ni kikundi cha uchechemuzi cha wajane nchini Côte d’Ivoire, akiandaa mlo kila usiku ili kusaidia wajane wanaoishi kwenye eneo lake.
Lia alinzisha nyumbani kwake Ergneti, Georgia makumbusho ya muda kuhusu vita vya mwaka 2008 nchini mwao.
Makumbusho hayo yanajumuisha picha, vifaa na mambo mengine yahusianayo na vita.
Makumbusho yako kwenye handaki la nyumba yake, ikiwa ni mita chahe kutoka mpaka wa eneo la kiutawala.
Chumba cha darasa kilichofurika wanafunzi wapatao 120 wenye umri wa kati ya miaka 11 hadi 14 kwenye shule ya wavulana mji mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR, Bangui.
Mwalimu wao, Bwana Basile anawaonesha picha ya watoto wa kiislamu wakionewa na watoto wa kikristo na halikadhalika watoto wa kiislamu wakiwaonea watoto wa kikristo na kuwaulia, “Je hii in sawa au si sawa?” na wanafunzi kwa pamoja wanasema, “si sawa!”
Wakati wa vita vya mwaka 2008 nchini Georgia, Madona na mumewe walitekwa nyara. Mumewe aliuawa na Madona alikimbilia Koda akiwa na wanawe watatu.
Punde alianzisha shirika la wanawake linalosaidia mikakati mbalimbali ya kuinua wanawake wakimbizi kijamii na kiuchumi
Chantal, Mratibu wa shirika la kiraia la wanawake, Planète Femmes, anashirikiana na wanawake manusura wa ukatili wa kijinsia kutoka pande zote zinazokinzana nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati
Hukutana mara moja kwa wiki ili wanawake waweze kubadilishana simulizi zao na kusaidiana
“Maisha baada ya Vita: Simulizi kama zilivyoelezwa kwa ICC na manusura wa uhalifu mbaya zaidi wa kivita duniani” zinaadhimisha miaka 20 ya ICC tarehe 1 Julai mwaka 2022.
Maonesho ya picha hizo yako kwenye ushoroba wa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa New York, Marekani hadi Julai 29, 2022.