
Chifu mwanamke wa kata ya Matembo Bi Kasoki Vaitsola Nadine akitoa maelezo ya awali kwa walinda amani wanawake wa kikosi cha 8 cha Tanzania, TANZBATT_8 katika kikosi cha kujibu mashambulizi, FIB cha ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini DRC, MONUSCO, kabla ya kuanza kwa mkutano kati yao.

Mlinda amani kutoka Tanzania (TANZBATT_8) Koplo Johnson Ndohele akimsikiliza msaidizi wa Chifu wa Kata ya Ngadi Bwana Faraja Mbusa muda mfupi baada ya kumalizika kwa mkutano wa walinda amani wanawake kutoka Tanzania wanaohudumu katika Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini DRC, MONUSCO.

Kiongozi wa walinda amani wanawake katika kikundi cha 8, TANZBATT_8 wanaohudumu katika ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini DRC, MONUSCO, Meja Praksidia Rwekamwa akizungumza na wanawake (hawako pichani) kutoka katika kata za Ngadi, Matembo na Nzuma mjini Beni jimboni Kivu Kaskazini kwa lengo la kujitambulisha na kujua changamoto zinazowakabili wanawake wa maeneo hayo

Walinda amani wanawake kutoka Tanzania (TANZBATT_8) wanaohudumu katika Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini DRC, MONUSCO wakijadiliana na wanawake kutoka katika kata za Ngadi, Matembo na Nzuma mjini Beni,jimboni Kivu Kaskazini juu ya changamoto zinazowakabili.