
Walinda amani kutoka Tanzani wanaohudumu kwenye moango wa MONUSCO katika kikosi cha FIB wakiwa Mavivi, mji wa Beni nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo, DRC wakiwaelezea wanawake wakulima kuhusu kilimo endelevu cha mboga kwa ajili ya matumizi yao lakini pia kuuza. Kufikia sasa kaya 25 Mavivi, zimenufaika kutokana na mradi wa kulima mboga.

Ukosefu wa usalama katika jimbo la Kivu Kaskazini kumesababisha wanawake kutumbukia katika umaskini kwani hawakuweza tena kushiriki shughuli za kujipatia kipato. Lakini kufuatia uwepo wa FIB kutoka Tanzania, wanawake wanapata stadi ikiwemo ushonaji ambapo mllinda amani kama huyu anatoa mafunzo kwa mkazi wa Mavivi, eneo la Beni kuhusujinsi ya kushona nguo.

Walinda amani wanawake kutoka Tanzania wakifanya doria katika eneo la Mavivi wakizungumza na wanawake mashinani katika jimbo la kivu kasakzini mji wa Beni moja ya maeneo yaliyoghubikwa na vita. Kikosi cha MONUSCO cha FIB cha walinda amani wanawake kutoka Tanzania kimewezesha wanawake kuendelea na shughuli zao za kila siku ikiwemo kuhudhuria kliniki katika maeneo wanakoishi.