POPO WANAENEZA VIRUSI VYA EBOLA AU LA?


Daktari akiwa na popo kwenye maabara ambapo popo huyu anachunguzwa kubaini iwapo ana virusi vya Ebola au la. Popo wamekuwa wanadaiwa kubeba virusi na kuvieneza na hivyo kuleta madhara kwa binadamu.

Daktari akiwa ndani ya maabara akichunguza iwapo damu ya popo ina virusi vya ebola. Ugonjwa wa Ebola ulileta madhara makubwa nchini Sierra Leone. Na Madaktari hawa ni matokeo ya mafunzo yaliyotolewa na shirika la nishati ya atomiki duniani IAEA na shirika la chakula na kilimo duniani, FAO kwa wataalamu kutoka mataifa 7 ya Afrika kuhusu matumizi ya teknolojia ya nyuklia kubaini virusi kwa popo.

Vifaa ambavyo vinatumiwa katika utafiti wa virusi vya Ebola nchini Sierra Leone vinaanikwa nje ili vikauke na pia kuondoa makali ya minunurisho. Kwani hutumia teknolojia ya nyuklia katika utafiti huo.

Kwa kuwa wataalamu wanaosaka virusi hutumia teknolojia ya nyuklia na kuwa katika mazingira ya yaliyosheheni vijidudu pamoja na popo wanaochunguzwa, wataalamu hao hulazimika kujikinga kwa vifaa maalum ikiwemo mavazi, barakoa na glovu.

Watafiti katika kituo cha Njala Sierra Leone wakichukua damu ya popo ili ifanyiwe uchunguzi kwa sababu inadaiwa kuwa popo walikuwa chanzo cha kuenea kwa virusi vya Ebola kwenye mlipuko wa ugonjwa huo mwaka 2014. Hii ni mwezi Oktoba mwaka huu wa 2018.

Wataalamu wa mifugo na Wanyamapori kutoka nchi saba za kiafrika wakisikiliza kwa makini wanachoelezwa katika mafunzo ya jinsi ya kutafiti virusi vya Ebola kwa popo. Yaelezwa kuwa popo anaweza kueneza virusi hivyo.