Guinea na ulinzi wa amani nchini Mali

Msafara wa walinda amani wa Umoja wa Mataifa kutoka Guinea wakiwa Kidal nchini Mali

Wakiwa na kambi yao Kidal kaskazini mwa Mali, walinda amani kutoka Guinea ni askari wapatao 868.

Katika kikosi cha MINUSMA kinachoundwa na askari 868, wanawake ni 16.

Mlinda amani mwanamke kutoka Guinea akiwa kazini katika kambi ya walinda amani wa Umoja wa Mataifa Kidal kaskazini mwa Mali.

Mlinda amani kutoka Guinea akihudumu nchini Mali hapa akiwa katika eneo la kazi.

Askari wa Guinea kutoka kikosi cha vilipuzi akiikagua barabara katika eneo la Kidal huko Mali.

Walinda amani kutoka Guinea, wanasaidia katika kutafuta na kutegua vilipuzi vilivyoachwa katika maeneo mbalimbali vikihatarisha maisha ya wananchi.

Askari wa MINUSMA kutoka Guinea wakiwa katika lindo.