KOFI NA HARAKATI ZA AMANI


Kofi Annan, Katibu Mkuu wa UN akikaribishwa na Rais Daniel arap Moi wa Kenya kwenye ikulu mjini Nairobi wakati alipotembelea nchi hiyo tarehe 4 mwezi Mei mwaka 1998.

Ikulu jijini Dar es salaam nchini Tanzania Kofi Annan, Katibu Mkuu wa UN na mkewe Nane Annan walipotembelea Tanzania tarehe 6 mwezi Mei mwaka 1998 na kukutana na wenyeji wao Rais Benjamin Mkapa na mkewe Bi. Anna Mkapa.

Tarehe 5 Machi mwaka 1997, Katibu Mkuu wa UN Kofi Annan (kulia) akisalimiana na Yasser Arafat, Mwenyekiti wa Kamati tendaji ya chama cha ukombozi wa Palestina, PLO.

Tarehe 4 Julai 2006, Katibu Mkuu wa UN Kofi Annan akikutana na Rais wa Liberia Ellen Johnson- Sirleaf mjini Monrovia, Liberia

Tarehe 24 Machi 1997, Kofi Annan, Katibu Mkuu wa UN akikutana na Jonas Savimbi, kiongozi wa UNITA kwenye uwanja wa ndege wa Bailundo wakati Bwana Annan akiwa katika ziara ya siku 9 Afrika Kusini, Namibia na Togo, ziara aliyoanza tarehe 18 mwezi Machi.

Tarehe 19 Januari 2000 Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan (wa pili kulia) alikutana na msuluhishi, msuluhishi mkuu wa mzozo wa Burundi kupitia mazungumzo ya Arusha, Nelson Mandela (wa tatu kutoka kulia) kwenye makao makuu ya UN mjini New York, Marekani.

Mwaka 2002 wakati wa sherehe za uhuru wa Timor Mashariki, Katibu Mkuu wa UN Kofi Annan (kulia) akiwa amesimama wakati bendera ya Umoja wa Mataifa ilipokuwa inateremshwa ili kuanza shamrashamra za uhuru kwenye mji mkuu Dili. Bwana Annan alikuwa mstari wa mbele kufanikisha hatua hii.