![Walinda amani kutoka China wakiwa kwenye gwaride nchini Mali Walinda amani kutoka China wakiwa kwenye gwaride nchini Mali](https://global.unitednations.entermediadb.net/assets/mediadb/services/module/asset/downloads/preset/assets/2018/05/25-05-2018-MINUSMA-China-25623402367.jpg/image770x420cropped.jpg)
Walinda amani wa UN walitumwa Mali 2013, kufuatia hatua ya waasi ya kujaribu kutwaa eneo la kaskazini mwa nchi hiyo. Jukumu kuu la ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Mali, MINUSMA ni kusaidia kuendeleza mkataba wa amani ulio katika hali tete kwa kushirikiana na mamlaka za serikali na pia kulinda raia.
![Polisi wa UN wakiwa doriani huko Timbuktu kaskazini mwa Mali. Hii ni mwaka 2017 wakilenga kusaidia usalama wa raia. Polisi wa UN wakiwa doriani huko Timbuktu kaskazini mwa Mali. Hii ni mwaka 2017 wakilenga kusaidia usalama wa raia.](https://global.unitednations.entermediadb.net/assets/mediadb/services/module/asset/downloads/preset/assets/2018/05/25-05-2018-Mali-MINUSMA-02.jpg/image770x420cropped.jpg)
Takriban watendaji 15,000 wakiwemo wanajeshi, , polisi na wafanyakazi wa kiraia ndio wanafanya kazi na ujumbe huo. Polisi wa Umoja wa Mataifa wajulikanao kama UNPOL (ichani) wakiwa kwenye doria Timbuktu, kaskazini mwa Mali wakitoa ulinzi wa raia mjini humo dhidi ya vitisho vya kigaidi na uhalifu wa kupangwa.
![Msafara wa UN kati ya Gao na Kidal kaskazini mwa Mali. Februari 2017 Msafara wa UN kati ya Gao na Kidal kaskazini mwa Mali. Februari 2017](https://global.unitednations.entermediadb.net/assets/mediadb/services/module/asset/downloads/preset/assets/2018/05/25-05-2018-Mali-MINUSMA-01.jpg/image770x420cropped.jpg)
Ujumbe huo hufanya doria katika maeneo makubwa ili kulinda na kujenga imani miongoni mwa raia wanaokabiliana na vitisho na pia kuyafanya maeneo yaliyo ndani zaidi mwa nchi kuwa tulivu. Pichani ni magari ya UN yakiwa kwenye msafara kati ya Gao na Kidal kaskazini mwa Mali.
![Baada ya kupata mafunzo kutoka UNMAS, walinda amani hawa kutoka Cambodia kwenye kikosi cha MINUSMA wako tayari kutegua mabomu na vilipuzi. Baada ya kupata mafunzo kutoka UNMAS, walinda amani hawa kutoka Cambodia kwenye kikosi cha MINUSMA wako tayari kutegua mabomu na vilipuzi.](https://global.unitednations.entermediadb.net/assets/mediadb/services/module/asset/downloads/preset/assets/2018/05/25-05-2018-Mali-MINUSMA-03.jpg/image770x420cropped.jpg)
Hali ya usalama bado ni tete. Mabomu ya kutegwa ardhini na vilipuzi vingine vimeua raia wengi wa Mali katika kipindi cha miaka michache iliyopita, kwa hivyo ujumbe huo mara kwa mara huondoa vilipuzi hivyo kama sehemu ya jukumu la kuwalinda raia.Hapa kikosi maalum cha kutegua mabomu kutoka Cambodia kikielekea Gao kikiwa ndani ya ndege ya Umoja wa Mataifa.
![Walinda amani wa MINUSMA wakizungumza na raia huko Gao, kaskazini-mashariki mwa Mali. Walinda amani wa MINUSMA wakizungumza na raia huko Gao, kaskazini-mashariki mwa Mali.](https://global.unitednations.entermediadb.net/assets/mediadb/services/module/asset/downloads/preset/assets/2018/03/03-27-2018-MINUSMA-Peacekeepers-02.jpg/image770x420cropped.jpg)
Walinda amani hushirikiana kwa karibu na raia kote nchini Mali. Katika kijiji cha Bara, kilichoko umbali wa kilomita 85 kutoka mji wa Gao, askari wa MINUSMA walio kwenye doria wanazungumza na wananchi kuhusu changamoto wanazokabiliana nazo. Makundi yenye misimamo mikali hulenga maeneo na kuteka wat una kuwaua.
![Ujumbe wa MINUSMA hushambuliwa mara kwa mara. Pichani kikosi kutoka Guinea kikiwa kimeweka lindo eneo la vilimani mjini Kidal. Ujumbe wa MINUSMA hushambuliwa mara kwa mara. Pichani kikosi kutoka Guinea kikiwa kimeweka lindo eneo la vilimani mjini Kidal.](https://global.unitednations.entermediadb.net/assets/mediadb/services/module/asset/downloads/preset/assets/2018/05/25-05-2018-Mali-MINUSMA-05.jpg/image770x420cropped.jpg)
Kulinda amani nchini Mali ni kazi ngumu na ya hatari na ujumbe unakabiliwa na vitisho la kila mara kutoka kwa magaidi. Takriban walinda amani 170 wamepoteza maisha yao katika kipindi cha miaka mitano iliyopita. Kikosi kutoka Guinea kiliweka kambi maeneo ya miinuko kuzunguka mji wa Kidal ili kuzuia magaidi kushambulia kambi ya MINUSMA.