Miaka 15 ya ulinzi wa amani wa UN Liberia


2003: Wapiganaji wa zamani wakiwasilisha silaha kwenye kambi ya Schieffelin, nje yam ji mkuu Monrovia, wakati wa kampeni ya upokonyaji silaha. Wakati wa operesheni nzima ya ulinzi wa amani Umoja wa Mataifa uliwapokonya silaha zaidi ya wapiganaji 100,000 na kukusanya silaha zaidi ya 21,000. Picha:UN/Astrid-Helene Meister

2005: Wapiga kura wa Liberia mjini Doe wakiwa wamepanga foleni katikati ya dimbwi la maji wakisubiri kupiga kura katika uchaguzi wa kwanza wa kidemokrasia tangu kumalizika vita vya wenyewe kwa wenyewe. Ellen Johnson Sirleaf alishinda uchaguzi huo baada ya kuru za duru ya pili na kuwa mwanamke wa kwanza kuchaguliwa kidemokrasia kuwa Rais barani Afrika. Picha :UN/Eric Kanalstein

2007: Kitengo cha wauguzi kwenye mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Liberria UNMIL, ambacho kinatoa huduma muhimu ya afya mbali ya ulinzi, hususan vijijini ambako Hakuna hospitali za kutosha. Picha: UN/Eric Kanalstein

2007: Kikosi cha India kwenye mpango wa Amani wa Umoja wa Mataifa kikijumuisha zaidi wanawake, kikibadilisha kofia zao na kuchukua kofia za blu za Umoja wa Mataifa, kilipowasili Monrovia kuanza kazi ya ulinzi wa amani. Idadi kubwa ya walinda Amani wanawake iliwachagiza wanawake Liberia kujiunga na sekta ya ulinzi ikiwemo jeshi la polisi la taifa. Picha: UN/Eric Kanalstein

2010: Walinda Amani kutoka Pakistan wakiwafundisha vijana wa Liberia kupanga tofali kama sehemu ya mpango wa mafunzo ya kazi yaliyokuwa yanatolewa na kikosi hicho Pakistani mjini Tubmanburg. Picha: UN/Staton Winter

2012: Mlinda amani kutoka Ghana akiwa katika doria wakati wa ziara ya maafisa wa Umoja wa Mataifa mjini Cestos . walinda amani takriban 16,000 kutoka nchi zaidi ya nchi 12 wameshiriki operesheni za UNMIL Liberia tangu mwaka 2003-2018