Kwa miaka mingi sasa Mongolia imekuwa ikitoa huduma za afya na pia wahudumu katika vituo vya afya kwenye mji wa Abkabiya uliopo katika mkoa wa Darfur, nchini Sudan. Katika hospitali hiyo yenye wahudumu 68, wanaume 34 na wanawake 34 chini ya usimamizi wa Umoja wa Mataifa, wafanya kazi hao hutoa huduma za dharura, huduma za upasuaji , kupima miguu, huduma za msingi za meno na kutibu majeraha . Pia hutoa huduma ya chanjo na hatua nyingine za upimaji. Mbali na kuwahudumia wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa, kitengo cha hospitali cha Kimongolia kinawahudumia zaidi ya wagonjwa 10,000 kutoka Sudan kusini.
Tangu mwaka 2003, zaidi ya askari walinda amani 14,000 kutoka Mongolia wametumika katika jumbe mbalimbali za Umoja wa Mataifa kote ulimwenguni. Sasa hivi Mongolia ina takribani asakari wa kulinda amani 900 ikiwemo kwenye ujumbe wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa Sudan Kusini UNMISS, huko Abyei UNISFA, Darfur UNAMID, huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo MONUSCO na ukanda wa magharibi mwa Afrika.
Mwezi Mei mwaka 2017, zaidi ya askari walinda amani 850 kutoka Mongolia walitunukiwa medali za Umoja wa Mataifa kwa kazi nzuri ya kujitolea na huduma yao katika ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo UNMISS, na mwakilishi wa ujumbe huo, David Shearer.
Bwana Sheare alinukuliwa akiwapongeza walinda amani hao kwa kusema "walinda amani kutoka Mongolia wameongoza tija kwa ustadi wao ambao tungependa kuona zaidi katika jitihada zetu za kulinda amani nchini Sudan Kusini,"
Wakati ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sierra Leone ulipofungwa, Baraza la Usalama liliamuru ujumbe wa Umoja wa Mataifa katika nchi jirani ya Liberia (UNMIL) kutoa usalama kwa wafungwa na Mahakama. Mongolia ilikubali na kutuma walinda amani wake mwanzoni mwa mwaka 2006. Kitengo cha Walinzi wa Kimongolia kilichofundishwa na chenye nidhamu ya kiwango cha kimataifa kilifanya kazi kwa ustadi wa hali ya juu na kumaliza muda wake pasi tashiwsi yoyote nchini humo.