
Lukas Moh kutoka kituo cha ACAKORO akiwapatia maelezo Irene na Carol waliokuwa na ndoto ya kucheza soka. Kupitia mradi, washiriki wanapatiwa pia sare za michezo. Tangu utotoni, Carol na Irene walikuwa na ndoto ya kucheza soka na wakiwa na umri wa miaka 19 ndoto yao ikaanza kutimia.

Carol Odour akipiga danadana kwenye kituo cha kukuza vipaji vya soka cha ACAKORO, Nairobi, Kenya. Kituo kina makocha zaidi ya 12. Kituo hiki pamoja na kutoa mafunzo ya soka, kinapatia washiriki stadi za ufundi, kisaikolojia, chakula wakiwa mafunzoni, fedha za usafiri, na karo ya mafunzo.

Irene Odour akiwa mazoezini na yeye ni golikipa. Hapa ni kwenye kituo cha kukuza vipaji vya soka cha ACAKORO, Nairobi, Kenya. Zaidi ya wanafunzi 1,150 wamenufaika na mradi huu wa ubia kati ya UNICEF na ACAKORO. Kabla ya kushiriki mradi huu, Carol na Irene hawakuwa wanaenda shuleni. Habari Picha hii ni safari yao kwenye kituo cha ACAKORO na mafunzo ya umakenika