
Walinda amani wa Umoja wa Mataifa walio kwenye kikosi cha kuchukua hatua haraka, QRF nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambao wanatoka Kenya wakisambaza lita 24,000 za maji katika taasisi mbalimbali ikiwemo shule za Tuungane na Mbalimasu, hospitali ya Bey pamoja na kambi ya wakimbizi wa ndani ya Mbalimasu kufuatia ukame mkali uliokumba eneo hili la jimbo la Kivu kaskazini.

Walinda amani wa Umoja wa Mataifa kutoka nchini Afrika kusini walio katika kikosi cha kujibu mashambulizi, FIB nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC wakimpakiza kwenye helikopta kutoka Beni hadi Goma jimboni Kivu Kaskazini, mmoja majeruhi watatu waliokuwa mahututi kufuatia shambulio la kigaidi tarehe 17 Januari 2023.

Walinda amani wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani, Cyprus, UNFICYP wakiongozwa na Meja Jenerali Ingrid Gjerde(Katikati) wametoa msaada kwenye taasisi ya wakfu wa Kemal Saraçoğlu na kituo cha marafiki wa nyumba ya watoto wa Nicosia. UNFICYP ulikusanya na kukabidhi katika kituo hicho zaidi ya dola 15,000 pamoja na misaada mingine waliyokusanya wakati wa likizo za mwisho wa mwaka 2022 za kusaidia zaidi ya watoto 100 wenye saratani pamoja na mahitaji maalum.

Mbali na kutumia magari na helikopta, Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani, Cyprus, UNFICYP pia hutumia baiskeli kufanya doria kwenye eneo la karibu na mto. Eneo hilo, ambalo pia huitwa ‘Mstari wa Kijani’, lina ukubwa wa takriban kilomita 180 katika kisiwa hicho. Katika baadhi ya maeneo ya Nicosia eneo hilo lina upana mdogo na wakati maeneo mengine ni kilometa chache tu ndio zina upana mkubwa hivyo doria zinaweza kufanyika kwa kutumai baiskeli.

Zaidi ya wafanyakazi wa kiraia 14,000 wanahudumu katika operesheni za Ulinzi wa Amani za Umoja wa Mataifa duniani. Pichani ni Afisa wa Haki za Binadamu, Fadimata Yattara, mfanyakazi wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kuweka utulivu nchini Mali, MINUSMA, akizungumza na mkazi wa Menaka nchini humo.

Mara kwa mara, walinda amani wa mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Lebanon UNIFIL hutembelea shule kuzungumza na wanafunzi kuhusu jukumu la misheni nchini Lebanon Kusini. Lengo ni kukitambulisha kizazi kipya kwenye misheni hiyo ili waweze kuelewa vyema kile ambacho walinda amani wanafanya kusini mwa Lebanon na kwa nini wako hapa.