Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Neno La Wiki

Neno la wiki: Kizazi

Wiki hii tunaangazia neno “Kizazi” na mchambuzi wetu ni Onni Sigalla, Mhariri Mwandamizi, katika Baraza la Kiswahili la Taifa, BAKITA, nchini Tanzania.

Bwana Sigalla anasema neno hili lina maana zaidi ya moja.  Ungana naye akuchambulie...

(Sauti ya Bw. Sigalla)

Neno la wiki_Maafikiano na Mkinzano

Katika neno la wiki hii leo tunaangazia neno “Maafikiano” na “Mkinzano”.  Mchambuzi wetu  ni Nuhu Zuberi Bakari, ambaye ni Naibu Mwenyekiti wa masuala ya mawasiliano kwenye Chama cha  Kiswahili cha Taifa nchini Kenya, CHAKITA.

Nuhu anasema neno "maafikiano" ni pale ambapo watu wawili au watatu wanashirikiana kimawazo katika mchango wao kuhusu jambo fulani na "Mkinzano" linamaanisha hakuna maelewano au watu wanatofoutiana kimawazo kabisa kuhusu jabo fulani.  Ungane naye usikilize uxhambuzi zaidi...

Neno la wiki: Likiza

Wiki hii tunaangazia neno "Likizai" na mchambuzi wetu ni Onni Sigalla, Mhariri Mwandamizi, katika Baraza la Kiswahili la Taifa, BAKITA, nchini Tanzania. Je, neno hili lina maana ngapi?

Bwana Sigalla ansema neno Likiza lina maana zaidi ya moja, la kwanza ni kumpa mtoto mchanga ambaye bado ananyonyeshwa chakula kingine mbali na maziwa ya mama ili aanze kuzoea. Ya pili ni kusitisha au kumpumzisha mtu kufanya jambo ambalo amekuwa akifanya

Neno la wiki: Utengamano na Utengano

Katika neno la wiki hii leo tunaangazia neno "Utengamano" na "Utengano".  Mchambuzi wetu  ni Nuhu Zuberi Bakari, ambaye ni Naibu Mwenyekiti wa masuala ya mawasiliano kwenye Chama cha  Kiswahili cha Taifa nchini Kenya, CHAKITA.

Nuhu anasema utengamano ni hali kuwa kwa pamojan au kushirikiana, na utengano ni kinyume cha utengamano, yaani hali ya kutokuwepo pamoja, iwe kimawazo au kiuhalisia...

Neno la wiki: Zawadi

Wiki hii tunaangazia neno “Zawadi” na mchambuzi wetu ni Onni Sigalla, Mhariri Mwandamizi, katika Baraza la Kiswahili la Taifa, BAKITA, nchini Tanzania.

Je, neno hili lina maana ngapi?  Bwana Sigalla anakuchambualia....

(Sauti ya Bwana Sigalla)

Neno la wiki : Mtagusano

Katika neno la wiki hii leo tunaangazia neno “Mtagusano” Mchambuzi wetu  ni Nuhu Zuberi Bakari, ambaye ni Naibu Mwenyekiti wa masuala ya mawasiliano kwenye Chama cha  Kiswahili cha Taifa nchini Kenya, CHAKITA.

Nuhu anasema neno Mtagusano ni ushirikiano wa watu wawili au zaidi katika kujadili jambo fulani au katika kitendo chochote, watu hawa wakiwa na hoja za kufanana au mawazo ya kulingana.

Neno la wiki - Matamata

Wiki hii tunaangazia neno "Matamata" na mchambuzi wetu ni Onni Sigalla, Mhariri Mwandamizi, katika Baraza la Kiswahili la Taifa, BAKITA, nchini Tanzania.

Bwana Sigalla anasema neno "Matamata" ni hali ya kupepesuka aliyo nayo mtoto anayejifunza kutembea, ama mtu mzima ambaye ni mgonjwa na anajipa mazoezi ya kutembea polepole.  Ameongeza kuwa neno hili haina uhusiano na na neno "kujikongoja".

Neno la Wiki: Mlipuko na Mkurupuko

Katika neno la wiki hii leo tunaangazia maneno "Mlipuko" na "Mkurupuko" Mchambuzi wetu  ni Nuhu Zuberi Bakari, ambaye ni Naibu Mwenyekiti wa masuala ya mawasiliano kwenye Chama cha  Kiswahili cha Taifa nchini Kenya, CHAKITA.

Nuhu anasema neno "mlipuko" ni sauti ya ghafla ya kutisha ambayo inayotokana na moto au upasuaji ya mti na mengineyo, na neno "Mkurupuko" inatokana na neno kurupuka, ambalo linamaanisha kuamka kwa ghafla ama kutekeleza kitendo fulani kwa kushtukia au bila ya kupanga.

Neno la wiki: Sogi

Wiki hii tunaangazia neno “Sogi” na mchambuzi wetu ni Onni Sigalla, Mhariri Mwandamizi, katika Baraza la Kiswahili la Taifa, BAKITA, nchini Tanzania.

Bwana Sigalla anasema Sogi ni mifuko miwili anayebebeshwa punda, moja kila upande ambayo hutumiwa kubeba mizigo ndani yake.