Neno la wiki : Mtagusano
Pakua
Katika neno la wiki hii leo tunaangazia neno “Mtagusano” Mchambuzi wetu ni Nuhu Zuberi Bakari, ambaye ni Naibu Mwenyekiti wa masuala ya mawasiliano kwenye Chama cha Kiswahili cha Taifa nchini Kenya, CHAKITA.
Nuhu anasema neno Mtagusano ni ushirikiano wa watu wawili au zaidi katika kujadili jambo fulani au katika kitendo chochote, watu hawa wakiwa na hoja za kufanana au mawazo ya kulingana.