Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Neno La Wiki

Neno la Wiki- Madhabahu

Wiki hii tunaangazia neno "Madhabahu" na mchambuzi wetu ni Onni Sigalla Mhariri Mwandamizi, katika Baraza la Kiswahili la Taifa, BAKITA, nchini Tanzania.

Bwana Sigalla anasema neno hilo lina maana tatu. Maana ya kwanza ikiangazia pahala takatifu, maana ya pili ni pahala pa kufanyia tambiko na maana ya tatu ni pahala pa kuchinjia wanyama.

Neno la Wiki- maneno yanayotumika kama kitenzi

Katika neno la wiki Februari 17 tunachambua maneno yanayotumika kama kitenzi, mchambuzi wetu leo ni, Nuhu Zuberi Bakari ambaye ni Naibu Mwenyekiti wa masuala ya mawasiliano kwenye Chama cha  Kiswahili cha Taifa nchini Kenya, CHAKITA.

Bwana Nuhu anasema kwamba kuna maneno yanyotumika kwenye lugha ya Kiswahili lakini hayapo ila tu yanatumika kihisi kama njia ya kusisitiza, anatolea matamshi ya baadhi ya maneno na jinsi matamshi yanaonyesha msisitizo

Neno la Wiki- Chelewa

Wiki hii tunaangazia neno Keneka na mchambuzi wetu ni Onni Sigalla Mhariri Mwandamizi, katika Baraza la Kiswahili la Taifa, BAKITA, nchini Tanzania.

Kulingana na Bwana Sigalla neno hili lina maana zaidi ya moja, kwanza kama nomino, ala ya mziki ya kienyeji yenye vijiwa vinavotiwa katika mkebe, nyingine ni kuwa nyuma na wakati na chelewa nyingine kama nomino ni hali anayoiona mlevi baada ya kulewa jana, jina jingine ni maluweluwe.

Neno la wiki- Yamkini/ Yakini

Katika neno la wiki Februari 3 tunachambua maneno yamkini na yakini, mchambuzi wetu leo ni, Nuhu Zuberi Bakari ambaye ni Naibu Mwenyekiti wa masuala ya mawasiliano kwenye Chama cha  Kiswahili cha Taifa nchini Kenya, CHAKITA.

Bwana Bakari anasema kwamba neno yamkini maana yake kutokuwa na uhakika na jambo au kitu kufanyika, pengine, labda. Anaongeza kwamba asili ya neno hili ni kiarabu na kwa hiyo watu wa Pwani iwe Kenya au Tanzania wanatumia neno yumkini. Kinyume cha yamkini ni yakini, yakini ina maana ya uhakika.