Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Neno La Wiki

Neno la Wiki- Gidamu

Wiki hii tunaangazia neno "Gidamu" na mchambuzi wetu ni Onni Sigalla, Mhariri Mwandamizi, katika Baraza la Kiswahili la Taifa, BAKITA, nchini Tanzania.

Bwana Sigalla anasema neno hili lina maanza tatu, ungana naye uapte uchambuzi kwa kina.

Neno la wiki: Shimizi

Katika neno la wiki hii leo tunaangazia neno "Shimizi".  Mchambuzi wetu  ni Nuhu Zuberi Bakari, ambaye ni Naibu Mwenyekiti wa masuala ya mawasiliano kwenye Chama cha  Kiswahili cha Taifa nchini Kenya, CHAKITA.

Nuhu anasema Shimizi ni vazi ya siri ambayo wanawake wanalivalia ndani ya nguo ama wanavaa wakati wanalala. Amesema ni aina fulani ya rinda inachovaliwa kwenye sehemu ya mabega hadi magotini....na anailinganisha na vesti inayovaliwa na wanaume..

Neno la wiki: Kizazi

Wiki hii tunaangazia neno “Kizazi” na mchambuzi wetu ni Onni Sigalla, Mhariri Mwandamizi, katika Baraza la Kiswahili la Taifa, BAKITA, nchini Tanzania.

Bwana Sigalla anasema neno hili lina maana zaidi ya moja.  Ungana naye akuchambulie...

(Sauti ya Bw. Sigalla)

Neno la wiki_Maafikiano na Mkinzano

Katika neno la wiki hii leo tunaangazia neno “Maafikiano” na “Mkinzano”.  Mchambuzi wetu  ni Nuhu Zuberi Bakari, ambaye ni Naibu Mwenyekiti wa masuala ya mawasiliano kwenye Chama cha  Kiswahili cha Taifa nchini Kenya, CHAKITA.

Nuhu anasema neno "maafikiano" ni pale ambapo watu wawili au watatu wanashirikiana kimawazo katika mchango wao kuhusu jambo fulani na "Mkinzano" linamaanisha hakuna maelewano au watu wanatofoutiana kimawazo kabisa kuhusu jabo fulani.  Ungane naye usikilize uxhambuzi zaidi...