Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Neno La Wiki

Neno la wiki: Aghalabu

Wiki hii tunaangazia neno “Aghalabu” na mchambuzi wetu ni Onni Sigalla Mhariri Mwandamizi, katika Baraza la Kiswahili la Taifa, BAKITA, nchini Tanzania.

Aghalab ni kama kielezi na inatumika kumaanisha "mara nyingi, au kwa kawaida au mara kwa mara".  Mfano ya matumizi ya neno Aghalab kwa sentensi ni "Nyota nyingi aghalab huonekana usiku" Neno hili lina vinyume vyake kwa mfano nadra, adhimu au mara chache.

Watu wengine hutumia neno hili kimakosa, mara nyingi kumaanisha mara chahe au nadra

Neno la wiki- Keneka

Wiki hii tunaangazia neno Keneka na mchambuzi wetu ni Onni Sigalla Mhariri Mwandamizi, katika Baraza la Kiswahili la Taifa, BAKITA, nchini Tanzania.

Kulingana na Bwana Sigalla, keneka ina maana ya kugeuza maji kuwa mvuke kwa kuchemsha na kisha kukusanya matone ya mvuke uliopita na kuwa maji maji.

Huu ni mchakato wa kisayansi ambao unafanyika ili watu waweza kupata maji yaliyoondolewa ikiwemo chumvi ili kupata maji safi ya kunywa.

Neno la wiki- Tovuti na Wavuti

Katika neno la wiki Januari 6 tunachambua maneno Tovuti na Wavuti, mchambuzi wetu leo ni, Nuhu Zuberi Bakari ambaye ni Naibu Mwenyekiti wa masuala ya mawasiliano kwenye Chama cha  Kiswahili cha Taifa nchini Kenya, CHAKITA.

Bwana Nuhu anasema kwamba maneno haya yanatumika vivyo sivyo kwani Tovuti ni intaneti na wavuti ni website.