Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Neno La Wiki

Neno la wiki: Kichinjamimba

Wiki hii tunaangazia neno "Kichinjamimba" na mchambuzi wetu ni Onni Sigalla, Mhariri Mwandamizi, katika Baraza la Kiswahili la Taifa, BAKITA, nchini Tanzania.

Bwana Sigalla anasema Kichinjamimba ni mtoto ambaye amezaliwa mwishoni kabisa katika idadi ya watoto wa mama.

Neno la wiki: Bwela Suti

Katika neno la wiki hii leo tunaangazia maneno "Bwela Suti".  Mchambuzi wetu  ni Nuhu Zuberi Bakari, ambaye ni Naibu Mwenyekiti wa masuala ya mawasiliano kwenye Chama cha  Kiswahili cha Taifa nchini Kenya, CHAKITA.

Nuhu anasema “Bwela Suti” ni "apron" au vazi analovaa mtu ili kuzuia uchafu wa mafuta ama vitu vyovyote vile kuharibu nguo zake, aghalabu au hususan hutumika jikoni, lakini pia linawezatumika katika mazingira mengine.

Neno la wiki: Harara

Wiki hii tunaangazia neno “Harara” na mchambuzi wetu ni Onni Sigalla, Mhariri Mwandamizi, katika Baraza la Kiswahili la Taifa, BAKITA, nchini Tanzania.

Bwana Sigalla anasema neno "Harara" lina maana nyingi, ya kwaza ni jinsi mtu anavyohisi kuwashwawashwa kwnye ngozi ya mwili, pili ni hali ya mtu kuwa na hasira mbaya ya ghafla, tatu ni hali ya mtu kutokwa na vipele kwenye ngozi, na ya nne ni mbambuko wa ngozi aghalabu kwa watoto au wanawake katika sehemu za mapaja kutokana na joto kali.

Neno la wiki: Kishida na Kibiriti Ngoma

Katika neno la wiki hii leo tunaangazia maneno “Kishida na Kibiriti Ngoma”.  Mchambuzi wetu  ni Nuhu Zuberi Bakari, ambaye ni Naibu Mwenyekiti wa masuala ya mawasiliano kwenye Chama cha  Kiswahili cha Taifa nchini Kenya, CHAKITA.

Nuhu anasema "Kishida" ni gauni kifupi au kirinda nyepesi kinachovaliwa usiku na mwanamke au msichana anapolala au kinachovaliwa ndani ya nguo, Kibiriti Ngoma ni "mini_skirt" au rinda fupi...