Vichwa vya Habari
Habari Moto Moto
Chaguo la Mhariri
Makala Maalum
Ukuaji wa Kiuchumi
Azimio la 5 la Manama limepitishwa hii leo huko Manama, mji mkuu wa Bahrain na washiriki wa Jukwaa la Kimataifa la Uwekezaji kwa Wajasiriamali likiwa na wito wa pamoja na mambo mengine likisihi jamii ya kimataifa na wadau wote katika sekta ya umma na binafsi kutumia nguvu ya ujasiriamali na uwekezaji katika nyanja zote za kiuchumi na kijamii kama kitovu cha kufanikisha Malengo ya Maendeleo Endelevu, SDGs kwa kupatia kipaumbele makundi maalum wakiwemo watu wenye ulemavu, wanawake, vijana na familia zinazohaha kutumia uwezo wa kuzalisha ili kujikimu kimaisha.
Habari kwa Picha
Sudan: Hadithi za maumivu na mateso katika mwaka wa vita
Soha na Suhaila Ahmed, mwenye umri wa miaka 12, ni mapacha kutoka jiji la Nyala huko Darfur. Vita nchini Sudan viliwalazimu kutoroka pamoja na mama yao na mdogo wao hadi mji wa Port Sudan ulioko mashariki ya mbali ya Sudan, katika safari ngumu ya mabasi na malori ya mizigo, iliyochukua umbali wa kilomita 2,360. Wasichana hao wawili, mama yao mgonjwa, na mdogo wao wa kiume walipata makazi ya muda katika bweni la wanafunzi katika Chuo Kikuu cha Port Sudan, wakisubiri kurejea Khartoum baada ya vita kuisha. Wasichana hao wawili wanangojea hatima isiyojulikana. Nilishangazwa na nguvu na uvumilivu wa wasichana hawa wawili na kwamba bado waliweza kutabasamu na kuwa na matumaini baada ya kupitia uzoefu huo mgumu.
Habari Nyinginezo
Malengo ya Maendeleo Endelevu
Suala la kuwekeza kwa wanawake wajasiriamali kwenye maeneo yenye mizozo duniani limepatiwa uzito hii leo mwishoni mwa mkutano wa 5 wa Umoja wa Mataifa kuhusu uwekezaji kwa wajasiriamali, WEIF 2024 huko Manama, mji mkuu wa Bahrain, jukwaa lililoratibiwa na Umoja wa Mataifa na wadau wake.
Ukuaji wa Kiuchumi
Ripoti ya Umoja wa Mataifa ya katikati ya mwaka ya hali na mtazamo wa uchumi wa Dunia kwa mwaka 2024 iliyotolewa leo inaonyesha matarajio ya kiuchumi duniani yameboreka tangu utabiri uliotolewa Januari 2024, lakini mtazamo ni wa matumaini yanayohitaji tahadhari.