Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakunga wafurahia kutoa huduma kwa wajawazito na watoto wachanga

Mkimbizi mjamzito wa Burundi mwenye umri wa miaka 23, amesimama nje ya nyumba yake katika kijiji cha Kalobeyei nchini Kenya.
© UNHCR/Samuel Otieno
Mkimbizi mjamzito wa Burundi mwenye umri wa miaka 23, amesimama nje ya nyumba yake katika kijiji cha Kalobeyei nchini Kenya.

Wakunga wafurahia kutoa huduma kwa wajawazito na watoto wachanga

Afya

Turkana nchini Kenya katika eneo la Kalobeyei ni makazi ya wakimbizi pamoja na jamii za wenyeji na huko Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR linatuunganisha na mkunga Jane Rose anaeleza namna anavyohakikisha anatoa huduma bora kwa wajawazito na watoto. 

Jane Rose Akwam, ni mkunga anayehudumia wajawazito pamoja na watoto wachanga, huduma ambayo inatolewa bure katika katika eneo hili la Kalobeyei.  Anasema, “Katika hospitali hii tunafanya kazi na jamii za wenyeji na wakimbizi, wanapokuja najitambulisha na kuwaeleza kazi yangu katika idara hii na pia nawaelezea kile ninachokuelezea ni kile ambacho hata mimi nilipitia.”

Wakati ulimwengu ulisherehekea siku ya wauguzi hapo na siku ya wakina mama hapo jana Mei 12, Rose anaeleza kile kinachompa furaha zaidi katika kazi yake hii ya ukunga.

“Ni furaha yangu ninapomuona mjamzito anapokuja kwa ajili ya kujifungua na mwisho wa siku anajifungua mtoto mwenye afya njema. Huduma hapa hutolewa bure ukitoa hata sumni bado itakurudia mwenyewe. Ni kama ninapotoa huduma kwa hawa wakina mama vyema najua zawadi yangu ipo pale.”