Habari kwa ufupi: Gaza, Sudan, Uchaguzi Mkuu DR Congo
Mashirika ya Umoja wa Mataifa leo yameendelea kusisitiza wito wa usitishwaji mapigano katika ukanda wa Gaza kwani hali inazidi kuwa mbaya kila uchao, lile la afya duniani WHO limesema timu yake ilifanikiwa kufika katika hospitali za Al Ahil Arab na Al Shifa Gaza kaskasini na uharibifu walioushuhudia hauelezeki.