UN yaanza utoaji chanjo kwa wahamiaji 7,500 waliokwama Yemen
Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji IOM leo limeanza kampeni ya chanjo ya COVID-19 kwa wahamiaji waliokwama nchini Yemen.
Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji IOM leo limeanza kampeni ya chanjo ya COVID-19 kwa wahamiaji waliokwama nchini Yemen.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres leo metangaza kumteua Bi Joyce Msuya wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa msaidizi wa wa Katibu Mkuu kwa masuala ya kibinadamu na naibu mratibu wa misaada ya dharura katika ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu masuala ya kibinadamu OCHA.
Rekodi mpya ya ya kutia hofu ya ongezeko la joto katika eneo la Arctic ya nyuzi joto 38C, au zaidi kidogo ya nyuzi joto 100 vipimo vya Fahrenheit, ilithibitishwa leo na shirika la hali ya hewa duniani WMO.
Idadi ya watu wenye njaa barani Afrika inaendelea kuongezeka, ikichochewa na uwepo wa migogoro, mabadiliko ya tabianchi na kuzorota kwa uchumi sababu nyingine mbalimbali ikiwemo pia janga la COVID-19. Imesema ripoti iliyotolewa leo na viongozi wa mashirika matatu ya kikanda barani Afrika ambayo yametoa wito wa kuchukua hatua zaidi juu ya mabadiliko ya mifumo ya kilimo.
Ushirikiano kati ya vyombo vya usalama ikiwemo polisi na FRDC ambalo ni Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC na vikosi vya walinda amani wa Umoja wa Mataifa wanaohudumu chini ya Mwavuli wa MONUSCO, umeendelea kuzaa matunda kwa kuwahakikishia usalama wananchi wa maeneo ya mashariki mwa DRC.
Wakimbizi 11,000 kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC waliokimbilia nchi jirani ya Uganda hivi karibuni kufuatia machafuko yanayoendelea Mashariki mwa DRC wameanza kurejea nyumbani kwa hiyari na kilichowasukuma ni usemi wa wahenga kuwa nyumbani ni nyumbani.
Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na idadi ya watu na afya ya uzazi duniani UNFPA, hii leo limezindua ombi maalum la dola milioni 835 likiwa ni ombi lake kubwa zaidi la kibinadamu ili liweze kuwafikia zaidi ya wanawake, wasichana na vijana milioni 54 katika nchi 61 mwakani 2022 kwa ajili ya kutoa msaada muhimu.
Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Ulimwenguni WHO na Hospitali ya Utafiti ya Watoto ya St. Jude hii wametangaza mipango ya kuanzisha jukwaa ambalo litaongeza kwa kasi upatikanaji wa dawa za saratani ya watoto duniani kote.
Kikosi cha wanajeshi kutoka Uingereza cha upelezi wa masafa marefu au LRRG chini ya Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kuweka amani nchini Mali, MINUSMA kinajivunia kuwa na askari wanawake miongoni mwao kwani kutokana na uwezo wao wa kuchapa kazi nyingi na kueleweka kwa wanajamii kirahisi. John Kibego anayo maelezo zaidi.
Ripoti mpya iliyotolewa na Shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni WHO inaonesha karibu vifo milioni saba vinaweza kuzuiwa ifikapo mwaka 2030, ikiwa nchi za kipato cha chini na cha kati zingewekeza chini ya dola moja kwa kila mwananchi kwa mwaka katika kuzuia na kutibu magonjwa yasiyoambukiza.