Msimu wa baridi, madhila zaidi ya wakimbizi wa Syria nchini Jordan
Miezi ya msimu wa baridi kali ikinyemelea, ni kumbukizi nyingine ya madhila kwa wakimbizi wa Syria waliosaka hifadhi Jordan ambao wengi wao wanaishi katika mazingira magumu wakati huu ambapo inaelezwa kuwa juhudi za shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR na wadau wake Jordan za kuwapatia vifaa vya kukabiliana na joto zinaonekana kuwa muhimu zaidi. Taarifa zaidi na Siraj Kalyango.