Upimaji VVUkwa wakati ni muhimili wa afya ya wafanyakazi- ILO
Katika takribani nchi 50 duniani imebainika kwamba maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi au VVU yanaongezeka na idadi ya vifo vitokanavyo na ugonjwa huo bado iko juu. Hayo ni kwa mujibu wa ripoti ya karibuni ya shirika la kazi duniani ILO iliyotolewa kuelekea siku ya ukimwi duniani itakayoadhimishwa kote duniani tarehe Mosi disemba.