Baraza la Usalama lauongezea muda ujumbe wa Umoja wa Mataifa Sahara Magharibi.
Wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, jumatano hii wamepitisha azimio la kuuongezea muda wa miezi sita zaidi ujumbe wa Umoja wa Mataifa huko ukanda wa Sahara ya Magharibi MINURSO huku pia wakiunga mkono juhudi za Katibu Mkuu Antonio Guterres na mwakilishi wake maalum za kuanzisha majadiliano kabla ya mwisho wa mwaka.